" DIWANI GLORIA IPOPO MWAMAJEMBA AONGOZA WANANCHI KUPANDA MITI ZAIDI YA 1,000 IWAMBI

DIWANI GLORIA IPOPO MWAMAJEMBA AONGOZA WANANCHI KUPANDA MITI ZAIDI YA 1,000 IWAMBI

Na Lydia Lugakila-Misalaba Media,

 Mbeya

Diwani wa Kata ya Iwambi, Mkoani Mbeya Gloria Ipopo Mwamajemba, ameongoza wananchi wa kata hiyo kushiriki zoezi la upandaji wa miti zaidi ya 1,000 katika mitaa mbalimbali ikiwemo Mayombo na Lumbila, ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan katika utunzaji wa mazingira.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo, mhe. Mwamajemba amewahimiza wananchi kuhakikisha kila mmoja anapanda miti katika makazi yake, akibainisha kuwa miti ina faida nyingi ikiwemo kuzalisha hewa safi ya oksijeni, kutoa kivuli, matunda, na kusaidia kupunguza ongezeko la joto duniani.

Aidha, amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwa kinara wa masuala ya mazingira nchini, na kuahidi kuwa kata ya Iwambi itaendelea kutekeleza kampeni ya upandaji miti kila mwaka ili kuifanya Iwambi kuwa na mazingira safi, mazuri na bora zaidi katika Jiji la Mbeya.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

 
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post