
Na Mapuli Kitina Misalaba
Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya
Shinyanga Mjini imeendelea na ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo
inayotekelezwa katika Manispaa ya Shinyanga, huku viongozi wakisisitiza umuhimu
wa kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati ili wananchi waweze kunufaika
na huduma zinazotarajiwa.
Ziara hiyo imefanyika leo Machi 11, 2026 ikiongozwa na
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Mhe. Anord Makombe, na kuhusisha
viongozi mbalimbali wa Manispaa na Wilaya.
Kamati imeanza ziara kwa kukagua ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa pamoja na
matundu ya vyoo katika Shule ya Awamu na Msingi Mwengi iliyopo mjini Shinyanga
ambapo Mwenyekiti Makombe amepongeza hatua za mradi huo.
Baada ya hapo, kamati imetembelea ujenzi wa zahanati katika Kijiji cha
Kolandoto, Kata ya Kolandoto ambapo Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga
Mjini, Mhe. Anord Makombe ameeleza kuwa zahanati hiyo ni muhimu kwa kuhakikisha
wananchi wanapata huduma za afya kwa haraka na karibu na makazi yao.
Kamati pia imekagua mradi wa upanuzi wa mtandao wa majisafi unaotekelezwa na
SHUWASA katika Kata ya Kolandoto na kwamba Mwenyekiti Makombe amesisitiza kuwa
maji safi ni muhimu kwa afya ya wananchi na maendeleo ya kijamii, hivyo mradi
lazima ukamilike kwa wakati na bila dosari za kiufundi.
Aidha, kamati hiyo imetembelea Shule ya Msingi Mwasena iliyopo Kata ya Kolandoto ambapo ilibaini kuwepo kwa changamoto ya upungufu wa madarasa shuleni hapo ambapo kutokana na hali hiyo, baadhi ya wanafunzi wanalazimika kusoma kwa kubanana katika darasa moja, huku darasa hilo likitumika na wanafunzi wa madarasa matatu tofauti kwa wakati mmoja.
Viongozi wa kamati hiyo wamesema hali hiyo inaathiri mazingira bora ya kujifunzia na kuahidi kufuatilia suala hilo kwa kushirikiana na mamlaka husika ili kutafuta suluhisho la haraka la kuongeza vyumba vya madarasa katika shule hiyo.
Ziara ilihusisha ukaguzi wa mradi wa TANESCO wa upanuzi wa umeme katika eneo la
Ibadakuli ambapo Samweli Jackson Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini
amepongeza juhudi za serikali na TANESCO huku Mwenyekiti Makombe akihimiza
uwajibikaji wa mara kwa mara ili mradi ukamilike kwa wakati na wananchi wapate
umeme wa uhakika.
Kamati pia imetembelea Shule ya Sekondari Rajani iliyopo Kata ya Ibadakuli ili
kukagua ujenzi wa mabweni mapya huku Makombe akisema mabweni ni muhimu kwa
kutoa hifadhi salama kwa wanafunzi na kuhamasisha malezi bora.
Ziara hiyo imemalizika kwa kukagua ujenzi wa jengo la wahandisi katika Manispaa
ya Shinyanga ambapo Mwenyekiti Makombe ameridhika na hatua ya mradi huo.
Ziara hiyo imehusisha viongozi mbalimbali: Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya
Shinyanga Mjini Mhe. Anord Makombe; Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya
ya Shinyanga Mjini Mzee Fue Mrindoko; Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga Said
Kitinga; Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Mhe. Salum Kitumbo; Kaimu
Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Doris Kibabi,
Samweli Jackson Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjinin a viongozi
wengine wakiwemo kutoka ofisi ya mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti Makombe amesisitiza kuwa Kamati itaendelea
kufuatilia kila mradi ili kuhakikisha malengo ya maendeleo kwa wananchi wa
Manispaa ya Shinyanga yanatimizwa kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.
Kaimu Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini ambaye
ni katibu wa jumuiya ya wazazi Wilaya ya Shinyanga mjini Bi. Doris Kibabi,
amepongeza utekelezaji wa miradi inayotekelezwa katika Manispaa ya Shinyanga.
Doris amebainisha kuwa miradi hiyo ni sehemu ya
utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi (CCM) chini ya Serikali ya Awamu ya
Sita ya Rais Samia Suluhu Hassan.
Amesema miradi hiyo, ikiwemo ujenzi wa madarasa,
mabweni na miundombinu ya majisafi, ni ishara ya dhahiri ya ahadi za chama
kufikiwa na kuleta maendeleo kwa wananchi wa Shinyanga huku akiwataka wananchi
kushirikiana na viongozi kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati na kwa
ubora unaotakiwa.
Ziara ya siku mbili ya Kamati ya Siasa ya CCM Wilaya
ya Shinyanga Mjini imehitimishwa leo ambapo viongozi wamesisitiza kuwa
ufuatiliaji wa miradi hiyo utaendelea ili kuhakikisha kila mradi unakamilika
kwa wakati, unaendana na viwango vya ubora na kwamba wananchi wanapata huduma
zinazotarajiwa.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Awali na Msingi Mwenge Manispaa ya Shinyanga Hassan Hemed akisoma taarifa fupi ya mradi huo.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Awali na Msingi Mwenge Manispaa ya Shinyanga Hassan Hemed akisoma taarifa fupi ya mradi huo.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Mhe. Anord Makombe akizungumza wakati wa ziara ya kukagua mradi katika shule ya msingi Mwenge mjini Shinyanga.
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Samweli Jackson akizungumza wakati wa ziara ya kukagua mradi wa TANESCO katika Kata ya Ibadakuli.
wenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Mzee Fue Mrindoko akizungumza ambapo amepongeza hatua nzuri ya mradi huo.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Mhe. Anord Makombe akipongeza weledi na kasi ya mradi huo kuwa unaridhisha.
Kaimu Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Doris Kibabi akizungumza wakati wa ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa mujibu wa Ilani ya CCM.🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254








































Post a Comment