Madereva wa pikipiki za kubeba abiria, maarufu kama bodaboda, mkoani Shinyanga wamepewa elimu na kuhamasishwa kupinga vitendo vya uharibifu au ukataji wa mabomba ya moshi (exhaust) kwenye pikipiki. Vitendo hivyo husababisha kelele na milipuko mikali ya sauti barabarani na katika mitaa mbalimbali.Akitoa elimu hiyo, Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga, Sajenti David Ndimila, amewataka madereva hao kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa kuhusu watu wanaohusika na vitendo vya kukata au kuharibu mabomba ya moshi ya pikipiki, ili waweze kubainika na kuchukuliwa hatua za kisheria.Sajenti Ndimila amesisitiza kuwa ushirikiano wa dhati kati ya madereva wa pikipiki na Jeshi la Polisi utasaidia kupunguza na hatimaye kutokomeza changamoto hiyo, ambayo imekuwa ikiongezeka kwa kasi katika mitaa mingi. Ameeleza kuwa kelele hizo zinaathiri afya za wananchi, hasa watu wenye matatizo ya moyo.Kwa upande wao, madereva wa pikipiki wamesema wako tayari kushirikiana na Jeshi la Polisi kuhakikisha wanazuia vitendo hivyo vya uharibifu wa mabomba ya moshi na kutoa taarifa za watu wanaotumia pikipiki zinazotoa milipuko ya sauti, ili kukomesha kabisa tatizo hilo.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment