Kuelekea ufunguzi wa mashindano ya Wailes Super Cup yatakayofanyika Mbinga Mjini tarehe 1 Aprili, klabu kongwe kutoka Songea, Majimaji Heroes, imeweka wazi dhamira yake ya kufanya makubwa katika michuano hiyo. Timu hiyo yenye historia kubwa ya soka katika ukanda wa kusini imesisitiza kuwa imejipanga kikamilifu kuhakikisha inaonyesha ushindani wa hali ya juu tangu mechi ya kwanza.Akizungumza kabla ya safari ya kuelekea Mbinga mvula amebainisha kuwa maandalizi yamekamilika, huku kikosi kikiwa katika hali nzuri kimwili na kiakili. Ameongeza kuwa Majimaji Heroes haitokwenda kushiriki tu, bali inalenga kutwaa ubingwa na kurejesha heshima ya klabu hiyo mbele ya mashabiki wake. Wachezaji pia wameonekana kuwa na morali kubwa wakiahidi kupambana kwa nguvu zote uwanjani.Mashindano hayo yanatarajiwa kuwa na ushindani mkali kutokana na ushiriki wa timu mbalimbali zenye viwango tofauti, lakini Majimaji Heroes wanaamini uzoefu wao utakuwa silaha muhimu. Mashabiki wa soka Songea na maeneo ya jirani wanasubiri kwa hamu kuona kama klabu hiyo itaweza kutimiza ahadi yake ya kurejea nyumbani na kombe.





SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment