Kituo cha redio cha Gold FM, kimeendelea
kujipambanua kama chachu ya maendeleo ya kijamii kwa kuhamasisha na kuinua
nafasi ya mwanamke tangu kuanzishwa kwake mwaka 2021.
Kupitia maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, kituo
hicho kimeendelea kufanya jukwaa maalum lijulikanalo kama “MWANAMKE CHUMA”,
lenye lengo la kuhamasisha, kuimarisha na kuwawezesha wanawake kwa kuwapa
nafasi ya kujifunza, kushirikiana, kuunganishwa na kutambulika katika jamii.
Mwaka huu, Tamasha la Mwanamke Chuma 2026 linatarajiwa
kufanyika Jumamosi, Aprili 11, 2026 katika Ukumbi wa Malex Hall, Kahama,
kuanzia saa 11 jioni, likiwa na kaulimbiu isemayo: “NGUVU YA UJASIRI”.
Tamasha hilo litapambwa na burudani kutoka kwa nguli
wa muziki wa Taarab nchini, Mzee Yusuph, huku mtaalamu wa maendeleo ya
familia na uchumi Dr. Chris Mauki akitoa elimu muhimu kwa wanawake na
wanaume. Aidha, mshereheshaji wa tukio hilo anatarajiwa kuwa Dr. Kumbuka,
ambaye ataleta hamasa na burudani ya kipekee jukwaani.
Mgeni rasmi katika tukio hilo anatarajiwa kuwa Mkuu wa
Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita, ambaye atahitimisha rasmi tamasha hilo
kubwa linalokusanya watu kutoka maeneo mbalimbali hasa ya Kanda ya Ziwa.
Mbali na burudani na elimu, tamasha hilo pia
litahusisha utoaji wa tuzo mbalimbali kwa wanawake waliofanya vizuri katika
nyanja tofauti, ikiwemo ubunifu na ushonaji, saluni bora, mwanamke mwenye
ushawishi, mjasiriamali bora na chipukizi, mpishi bora pamoja na kikundi bora.
Kwa mujibu wa waandaaji, tukio hilo linatarajiwa kuwa
jukwaa muhimu la kuibua vipaji, kuhamasisha ujasiri na kuongeza mchango wa
mwanamke katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
🎟️ Viingilio
vya tamasha hilo ni:
- Regular
– 30,000/=
- V.I.P
– 50,000/=
- Table
– 500,000/=
📞
Kwa mawasiliano na nafasi za kuhifadhi tiketi: 0744 357 578
Wananchi wote wa Kahama, Kanda ya Ziwa na maeneo ya
jirani wanahimizwa kujitokeza kwa wingi kushiriki tukio hili adhimu ambalo si
tu burudani, bali pia ni jukwaa la kuamsha ndoto, kuthubutu na kuonesha nguvu
ya mwanamke wa kisasa.
Usikose kuwa sehemu ya historia ya
Mwanamke Chuma 2026 – huu si usiku wa kawaida, ni usiku wa kuamsha uthubutu na
mafanikio!
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment