
NA DENIS MLOWE, IRINGA
Mwili wa aliyekuwa Waziri na Mbunge wa muda mrefu wa Ismani, marehemu William Lukuvi, uliwasili majira ya saa kumi na moia jioni katika Uwanja wa Ndege wa Nduli Airport na kupokelewa kwa majonzi, heshima na utulivu mkubwa na mamia ya wakazi wa mkoa wa Iringa pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali na chama.
Ndege iliyobeba mwili wa Lukuvi ilitua katika uwanja Nduli huku ikishuhudia baadhi ya viongozi wakitoa machozi kutokana na kifo cha nguli wa siasa nchini na mara tu ilipofungua milango, viongozi nbalimbali wa chama na serikali.wabunge wa maeneo jirani, pamoja na viongozi wa dini na waliupokea mwili huo kabla ya kupelekwa eneo maalum lililoandaliwa kwa ajili ya nyumbani kwake Gangilonga.
Wananchi waliokuwa wamefurika uwanjani hapo waliangua vilio na baadhi kushika mabango yaliyosheheni jumbe za kumuaga mwanasiasa huyo aliyelitumikia taifa kwa zaidi ya miongo mitatu Vijana, wanawake na wazee walionekana wakiwa na huzuni kubwa, wakimsifu Lukuvi kama kiongozi aliyekuwa karibu na wananchi na mwenye kuheshimu ahadi zake.
Baada ya mapokezi katika uwanja huo, msafara wa gari lililobeba mwili wake ulielekea katika makazi yake yaliyoko katika kata ya Gangilonga mtaa wa Lukuvindani ya manispaa ya Iringa kwa ajili ya mapumziko ambapo wananchi waliendelea kumiminika kutoa nyumbani kwake.
Ratiba ya mazishi inatarajiwa kuendelea kesho ambapo watasali katika kanisa la Roman Parokia ya Kihesa kwa ibada na shughuli za kuaga kabla ya mwili kupelekwa nyumbani Idodi kwa maziko. Mazingira ya Iringa ya barabarani yalioonwa na Full Shangwe Blog ni umati wa watu kusimama kando ya barabara kutaka kushuhudia kupita kwa mwili huo huku hali simanzi, ishara ya namna marehemu alivyogusa maisha ya watu wengi katika utumishi wake wa umma na siasa za Tanzania.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment