
Na Tonny Alphonce-Misalaba MediaMeneja wa NSSF mkoa wa Mwanza Emmanuel Kahensa amewataka wahitimu wa kidato Cha sita Mwanza Sekondari kujitofautisha na wengine Kwa kupata ufaulu wa juu.Amesema Kwa hali ilivyo hivi sasa watu wenye degree wapo wengi na Ili uwe tofauti unapaswa ufaulu wako uwe wa kiwango Cha juu.Kahensa mesema serikali Kwa upande wake chini ya Rais Samia Suluhu Hassan tayari imeweka mazingira mazuri ya elimu bora kuanzia elimu ya awali hadi chuo Kikuu hivyo ni lazima wapiganie matokeo mazuri.Upande wa changamoto za viti vya maabara na madawati Meneja Kahensa amesema NSSF Mwanza ipo tayari kutatua sehemu ya changamoto hizo.Awali akielezea mafanikio na changamoto za shule hiyo mkuu wa shule hiyo Sudi Rashid Gewa amesema changamoto kubwa waliyonayo Kwa hivi sasa ni ufinyu wa eneo la kuongeza majengo."Mgeni rasimi hapa tuna uhaba wa vyumba vya madarasa lakini hatuna eneo la kujenga,tuna uhaba wa matundu ya vyoo lakini pia hatuwezi kujenga Kwa Kuwa hatuna eneo,unachoweza kutusaidia ni madawati na viti vya maabara".alisema GewaGewa amesema Ili kuendana na miundombinu iliyopo shuleni hapo wamekuwa wakichukua wanafunzi kulingana na uwezo wa shule.Akizungumza Kwa niaba ya wahitimu wenzake mwanafunzi Mabuba Donald amesema matarajio yao ni kupata matokeo mazuri kwakuwa mazingira ya kusomea yalikuwa rafiki kwao.


SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment