" Senegal Mabingwa Halali wa AFCON

Senegal Mabingwa Halali wa AFCON

 

Senegal Ndio Mabingwa Halali wa AFCON

Kocha wa Timu ya Taifa ya Senegal, Pape Bouna Thiaw, amesema anaamini timu yake ndiyo Mabingwa halali wa Afrika licha ya kuvuliwa rasmi taji hilo mapema mwezi huu. Kauli hiyo imekuja kufuatia uamuzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), kuipatia Timu ya Taifa ya Morocco ubingwa huo.

Akizungumza kwa mara ya kwanza tangu uamuzi wa rufaa, Thiaw amesisitiza kuwa matokeo ya mashindano yanapaswa kuamuliwa uwanjani badala ya maamuzi ya nje ya uwanja. Amesema juhudi na kiwango walichoonesha Wachezaji wake ndani ya dimba haviwezi kufutwa kwa maamuzi ya kiutawala.

Uamuzi wa CAF ulitokana na tukio la Senegal kususia mchezo kwa dakika 14 wakati wa fainali iliyofanyika Rabat mwezi Januari. Hatua hiyo ilisababisha kubadilishwa kwa matokeo ya mchezo, na hatimaye Morocco kutangazwa mabingwa rasmi wa mashindano hayo.

Kwa sasa Senegal ipo Jijini Paris kwa maandalizi ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Taifa la Peru. Kabla ya mchezo huo, Thiaw amewataka Wachezaji wake kuweka umakini kwenye Soka na kuepuka mijadala ya utata inayohusu uamuzi wa CAF.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

 
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post