MKURUGENZI Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU)Chrispian Chalamila amekabidhi ripoti ya utendaji kazi wa taasisi hiyo kwa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ambapo pia ilifuatilia matumizi ya rasilimali za umma katika utekelezaji wa miradi 1,864, ambapo miradi 913 ilibainika kuwa na kasoro.
Akizungumza leo MachI 30,2026 Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akikabidhi ripoti hiyo ya TAKUKURU ya mwaka ya mwaka 2024/2025,Chalamila amesema kati ya miradi hiyo 913 yenye kasoro wakati miradi 66 imeanzishiwa uchunguzi.
Amesema idadi hiyo ni pungufu ikilinganishwa na miradi 92 iliyoanzishiwa uchunguzi mwaka 2023/24. “Idadi hii inaonesha kuwa miradi inayoanzishiwa uchunguzi inapunguahatua inayotokana na ufuatiliaji wa TAKUKURU katika utekelezaji wa miradi hiyo.
“Kwa ujumla, katika ufuatiliaji huu, tumebaini kuwepo kwa usimamizi dhaifu wa mikataba unaosababisha yafuatayo :Miradi kutekelezwa kwa kutozingatia matakwa ya mkataba husika,Wakandarasi kulipwa fedha kwa kazi ambazo hazikutekelezwa, kutokatwa kwa kodi ya zuio katika baadhi ya miradi.
“Pia ubora wa kazi na vifaa usioridhisha,kutozingatiwa kwa Sheria ya Ununuzi wa Ummaya Mwaka 2023; pamoja na Kufanyika kwa malipo - zaidi ya matakwa ya mkataba.
“Dosari zinazobainika katika ufuatiliaji wa matumizi ya rasilimali za umma katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo, zimekuwq zikijirudia.Nichukue fursa hii kuwakumbusha wote wenye dhamana ya kusimamia miradi hiyo wakiwemo makatibu wakuu,makatibu tawala na wakurugenzi wa halmashauri pamoja na taasisi za umma.”

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment