Dunia ya sasa haizungumzi lugha ya maneno matupu, bali inazungumza lugha ya matokeo na uaminifu, na hicho ndicho kinachoendelea kudhihirika katika ushirikiano kati ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Marekani.
Kaimu Balozi wa Marekani nchini, Andrew Lentz, ameweka wazi kuwa nchi yake itaendelea kuongeza nguvu katika Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Karume (KIST) kwa lengo moja tu: kuhakikisha kijana wa Kitanzania anapata ujuzi wa daraja la kwanza utakaomfanya awe tishio katika soko la ajira duniani.
Lentz amesema amevutiwa na jinsi chuo hicho kilivyopiga hatua, akisisitiza kuwa uaminifu uliojengwa kupitia mitaala inayokidhi mahitaji ya sasa ndiyo chachu ya Marekani kuendelea kutoa sapoti ya hali na mali.
Mkuu wa Chuo cha KIST, Dk. Mahmoud Abdulwahab Alawi, amebainisha kuwa matunda haya ya kuaminika yanatokana na mkakati wa makusudi wa kugeuza chuo hicho kuwa kiwanda cha wataalamu wanaoweza kujiajiri na kuwa wabunifu.
Chuo hicho kilichoasisiwa mwaka 1969 na Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Abeid Amani Karume, sasa kinazaliwa upya kikiwa na kozi za kisasa zinazomfanya mwanafunzi asitegemee tu kuajiriwa, bali awe mjasiriamali mwenye maarifa ya kisayansi. Huu ni ujumbe tosha kwa vijana kuwa wakati wa kusubiri miujiza umepita; sasa ni wakati wa kukumbatia elimu ya ufundi na teknolojia ambayo Marekani na wadau wengine wameamua kuipigia upatu kwa sababu wanaona matokeo yanayoshikika.
Kwa kijana wa Kitanzania, milango imefunguliwa na fursa zinamwagika kupitia ushirikiano huu wa kihistoria. Iwe ni kupitia ubunifu wa kiteknolojia hapo KIST unapokuwa na ujuzi unaohitajika sokoni unakuwa sumaku ya fursa .
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment