Na Paul Kayanda, GeitaKATIKA kijiji cha Ifugandi kilichopo Kata ya Busolwa, Wilayani Nyang’hwale mkoani Geita, chama kikuu cha ushirika wa wachimbaji madini kimeendelea kuleta mageuzi makubwa ya kiuchumi kupitia sekta ya madini, hususan uchimbaji wa dhahabu.Chini ya uongozi wa Mwenyekiti Mtingwa Mihambo, kwa kushirikiana na Mjumbe wa Bodi Masanja Philipo John pamoja wajumbe wengine, ushirika huo umefanikiwa kuwaunganisha wachimbaji wadogo na kuwawezesha kufanya shughuli zao kwa mfumo wa pamoja na wenye tija.Akizungumza na waandishi wa habari , Mwenyekiti Mihambo alisema kuwa ushirika huo umeongeza uzalishaji wa madini na kuinua kipato cha wanachama wake, jambo ambalo limechangia kuboresha maisha ya wananchi wa eneo hilo. “Kupitia ushirika wetu, wachimbaji wamepata sauti ya pamoja na uwezo wa kushiriki kikamilifu katika shughuli za uchumi Katika Kijiji chetu,” alisema Mihambo.Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali, kijiji cha Ifugandi ni miongoni mwa maeneo yanayochangia mapato ya wilaya kutokana na shughuli za uchimbaji dhahabu, ambapo pia biashara ndogondogo zimekua kwa kasi kufuatia uwepo wa machimbo kupitia ushirika huo. Aidha, wachimbaji wadogo katika eneo hilo wamekuwa na mchango mkubwa katika uchumi wa ndani licha ya changamoto za mara kwa mara zinazohusiana na uwekezaji na migogoro ya machimbo ya wawekezaji wakubwa.Mbali na wachimbaji, ushirika huo pia umewezesha makundi mbalimbali ya kijamii kunufaika kiuchumi ikiwemo kutengeneza ajira Nyingi Kwa Vijana na watu Wa lika mbalimbali Mfano ni Christina Pius, mama lishe wa Ifugandi, ambaye ameeleza jinsi shughuli za uchimbaji zilivyoongeza wateja na kukuza biashara yake. “Ushirika huu umetusaidia hata sisi wafanyabiashara wadogo kupata kipato cha uhakika,” alisema Pius.Mjumbe wa bodi, Masanja Philipo John, aliongeza kwa kusema kuwa ushirika umejikita pia katika kuwajengea wanachama uelewa wa sheria na taratibu za uchimbaji salama pamoja na kuhifadhi mazingira Ili shughuli hizo zifanyike Kwa tija zaidi.Mjumbe huyo ametumia ujio wa wanahabari hao kumshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Kwa kuyajali makundi ya Vijana na kuyapa kipaumbele kwenye sekta ya madini huku wakimbatiza kuwa ni mama wa Dhahabu."Kwa kweli tunamshukuru mama Samia Suluhu Hassan Kwa kutukumbuka sisi Vijana huyu ni mama wa Dhahabu kwani Katika kipindi chake hiki tumenufaika zaidi kupitia sekta ya madini, tumejiunga Katika kikundi Leo tunamiliki lesrni yetu ya uchimbaji Kwa hiyo Vijana waache kukaa vijiweni wanalalamika kukosa ajira waje huku tupambane na Dhahabu," amesema.Pamoja na mafanikio hayo, viongozi hao wameeleza kuwa bado wanakabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo miundombinu na migogoro ya mara kwa mara katika maeneo ya machimbo, lakini wameahidi kuendelea kushirikiana na serikali na wadau wengine ili kuboresha sekta hiyo.Uongozi wa chama kikundi cha ushirika Ifugandi umeendelea kuwa mfano wa mafanikio katika kuwawezesha wachimbaji wadogo na kuchangia maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika Wilaya ya Nyang’hwale na Mkoa wa Geita kwa ujumla.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254







Post a Comment