Ndoto ya Diwani wa Kata ya Itende, Mwl. Andambike Mwakyusa, ya kuinua kiwango cha elimu katika eneo lake imeanza kuzaa matunda, baada ya kuonesha dhamira ya dhati ya kushirikiana na walimu, wazazi na wanafunzi katika kuboresha mazingira ya kujifunzia.Hatua hiyo imejidhihirisha katika mahafali ya kwanza ya Kidato cha Sita ya Shule ya Sekondari Dr Tulia Ackson, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mkapa, Jijini Mbeya ambapo Diwani huyo amekuwa mgeni rasmi.Katika mahafali hayo,iliwasilishwa risala kutoka kwa walimu mkuu msaidizi wa shule hiyo iliyoeleza mafanikio pamoja na changamoto mbalimbali zinazoikabili shule hiyo, hususan tatizo la maji na ukosefu wa mashine ya kuchapisha mitihani.Kufuatia hali hiyo, Diwani Mwakyusa alihamasisha wazazi na wadau wa elimu kuchangia ili kufanikisha upatikanaji wa mashine hiyo pamoja na kuboresha upatikanaji wa maji shuleni.Katika kuchangia, Mhe. Mwakyusa alitoa shilingi milioni 1 pamoja na rola mbili za mipira ya maji. Walimu, viongozi wa kata na wazazi walichangia jumla ya shilingi 1,650,000 pamoja na rola moja ya mipira ya maji. Aidha, kiasi cha shilingi 600,000 kilichangwa kwa ajili ya kununua televisheni (TV) kwa matumizi ya wanafunzi. Diwani huyo pia aliahidi kuendelea kushirikiana na walimu katika kutatua changamoto nyingine zinazoikabili shule hiyo.Shule ya Sekondari Dr Tulia Ackson imefanikiwa kufanya mahafali yake ya kwanza ya Kidato cha Sita huku ikijivunia kulea vijana wenye nidhamu bora.Aidha Wanafunzi waliofanya vizuri kitaaluma pamoja na wale walioonyesha mabadiliko chanya ya kitabia walitunukiwa zawadi maalum.Akizungumza katika mahafali hayo, Diwani Mwakyusa alieleza kuwa anatamani kuona wanafunzi wanapata elimu bila vikwazo, na kusisitiza kuwa mashine ya kuchapisha mitihani itanunuliwa kabla ya wanafunzi kuanza mitihani ya taifa ili waweze kunufaika nayo. Pia aliwashukuru wazazi kwa ushirikiano wao mkubwa.“Moja ya mahitaji ya muda mrefu ambayo walimu wamekuwa wakiniomba kushirikiana nayo ni kuboresha taaluma" aliongeza kusema kiongozi huyo.Aidha, aliahidi kuendelea kuunga mkono shule hiyo pamoja na shule nyingine katika eneo lake ili kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bora bila vikwazo.Katika hatua nyingine, Diwani huyo alisisitiza umuhimu wa maadili kwa wanafunzi, akiwataka wazazi kuwalea watoto wao katika misingi bora ya maadili na dini ili kuepuka kuathiriwa na mienendo isiyofaa kutoka mitandaoni na mitaani.“Wazazi jitahidini watoto wenu waijue dini, wasiende kujiunga na mwelekeo wowote usiofaa,” alisisitiza.Kwa upande wake, Mkuu wa Shule ya Sekondari Dr Tulia Ackson, Daud Mwaijibe, alisema shule hiyo ilianza kupokea wanafunzi wa Kidato cha Sita mwaka 2024, ambao sasa wanahitimu mwaka 2026. Alieleza kuwa wanafunzi hao wamelelewa kitaaluma na kimaadili ili waweze kuwa na mchango chanya katika taifa.Aliongeza kuwa shule imekuwa ikiwatambua na kuwazawadia wanafunzi waliofanya vizuri katika nyanja mbalimbali, ikiwemo taaluma na mabadiliko chanya ya kitabia.“ Bila nidhamu na maadili mafanikio ya maisha ya baadaye yanakuwa magumu,” alisema Mwaijibe.Alibainisha kuwa shule imejipanga kuhakikisha wanafunzi wanapata matokeo mazuri katika mitihani yao, akieleza kuwa kuna mitihani mitatu ya majaribio kabla ya mtihani wa taifa ili kuwaandaa vizuri zaidi.Naye Mwalimu Mkuu Msaidizi, Dickson Kibiki, akisoma risala ya shule kwa mgeni rasmi, alisema shule hiyo imekuwa miongoni mwa zinazofanya vizuri katika ngazi ya wilaya, mkoa na taifa na aliwahimiza wazazi kuendelea kusisitiza nidhamu na utu kwa watoto wao.Kwa upande wao, baadhi ya wahitimu wa Kidato cha Sita, akiwemo Simon Danken na Mary Ngoi, walisema kuwa mafunzo ya nidhamu, maadili ya uvaaji, heshima na kumtumikia Mungu waliyoyapata shuleni hapo yatawasaidia kufikia ndoto zao za baadaye.SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment