Na Lydia Lugakila- Misalaba, Media MbeyaSemina ya neno la Mungu imefanyika Machi 31, 2026 katika Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Forest ya Kwanza, ikiongozwa na mtumishi wa Mungu, mchungaji Thobias Tambikeni.Katika semina hiyo, mchungaji Thobias Tambikeni aliwasihi waumini kuamini kuwa Mungu anajibu maombi kupitia misimamo yao binafsi waliyojiwekea.“Chukia mabaya yanapotendwa na mtu mwingine, kasirika usifurahi kwani huo ndio msimamo anaoutaka Mwenyezi Mungu. Onyesheni msimamo mnapotoka alisema mtumishi huyo".Amesema ni wakati sasa kwa waumini kutoka kwenye nguvu ya Tomaso, akieleza kuwa maisha ya kiroho hayahitaji kuweka kanuni bali kujitoa kwa vyovyote vile kwa Mungu.Mchungaji Thobias Tambikeni amesema kuwa waumini wanatakiwa kuipinga dhambi kwa gharama, kwa maneno na kwa matendo.Mtu huyo wa Mungu Pia amewahimiza waumini waliofanikiwa kufanya mambo makubwa kuendelea kumtumikia Mungu kwa bidii zaidi.“Semina hiyo imebeba ujumbe usemao ushindi kupitia nguvu ya msalaba.”
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment