" CHADEMA KANDA YA SERENGETI KUZINDUA UKARABATI WA OFISI

CHADEMA KANDA YA SERENGETI KUZINDUA UKARABATI WA OFISI

 Katibu wa CHADEMA Kanda ya Serengeti, Bwana Jackson Mnyawama, ametangaza kuwa chama hicho kinatarajia kufanya uzinduzi wa ukarabati wa ofisi ya kanda hiyo tarehe 26 Aprili mwaka huu.

Akizungumza kuhusu maandalizi hayo, Mnyawama amesema kuwa Kanda ya Serengeti inaundwa na mikoa mitatu ambayo ni Simiyu, Mara na Shinyanga, na kwamba ofisi ya kanda imekuwa ikihitaji ukarabati kwa muda mrefu, hivyo wameona ni wakati muafaka kuanza rasmi zoezi hilo.

Amesema uzinduzi huo utaongozwa na Mwenyekiti wa Kanda, Lucas Ngoto, huku viongozi wengine pamoja na wanachama kutoka mikoa yote ya kanda hiyo wakialikwa kuhudhuria kwa wingi ili kushuhudia na kushiriki katika hatua hiyo muhimu ya kuimarisha chama.

“Ofisi ni kielelezo cha uhai wa chama, hivyo kuwa na ofisi yenye mwonekano mzuri ni ishara kwamba chama kipo hai na kinaendelea kuimarika,” amesema Mnyawama.

Aidha, ametoa wito kwa wananchi na wanachama wa CHADEMA katika kanda hiyo kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo kwa kuchangia vifaa vya ujenzi, akisisitiza kuwa kila mmoja anaweza kutoa mchango wake kulingana na uwezo wake, ikiwemo tofali au mfuko wa saruji.

Kwa mujibu wa Mnyawama, ukarabati huo utahusisha ujenzi wa uzio kuzunguka ofisi, maboresho ya jengo lote, pamoja na ujenzi wa ukumbi wa ndani kwa ajili ya vikao. Pia, kutajengwa ukumbi mwingine katika kiwanja kilichopo nyuma ya ofisi kwa matumizi mbalimbali ya chama.

Kwa wale watakaoshindwa kufika katika uzinduzi huo, wamehimizwa kuchangia kupitia namba ya simu ya MPESA 0764 662 049 yenye jina CHADEMA Kanda ya Serengeti, au kupitia akaunti ya benki ya CRDB namba 015C765639500, yenye jina hilo hilo.

Mnyawama amesisitiza kuwa ushiriki wa pamoja wa wanachama na wananchi utasaidia kufanikisha azma ya kuwa na ofisi bora itakayochochea shughuli za chama katika kanda hiyo.

 SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post