
Katibu wa CHADEMA Kanda ya Serengeti, Bwana Jackson Mnyawama, ametangaza kuwa chama hicho kinatarajia kufanya uzinduzi wa ukarabati wa ofisi ya kanda hiyo tarehe 26 Aprili mwaka huu.
Akizungumza
kuhusu maandalizi hayo, Mnyawama amesema kuwa Kanda ya Serengeti inaundwa na
mikoa mitatu ambayo ni Simiyu, Mara na Shinyanga, na kwamba ofisi ya kanda
imekuwa ikihitaji ukarabati kwa muda mrefu, hivyo wameona ni wakati muafaka
kuanza rasmi zoezi hilo.
Amesema
uzinduzi huo utaongozwa na Mwenyekiti wa Kanda, Lucas Ngoto, huku viongozi
wengine pamoja na wanachama kutoka mikoa yote ya kanda hiyo wakialikwa
kuhudhuria kwa wingi ili kushuhudia na kushiriki katika hatua hiyo muhimu ya
kuimarisha chama.
“Ofisi ni
kielelezo cha uhai wa chama, hivyo kuwa na ofisi yenye mwonekano mzuri ni
ishara kwamba chama kipo hai na kinaendelea kuimarika,” amesema Mnyawama.
Aidha,
ametoa wito kwa wananchi na wanachama wa CHADEMA katika kanda hiyo kushiriki
kikamilifu katika zoezi hilo kwa kuchangia vifaa vya ujenzi, akisisitiza kuwa
kila mmoja anaweza kutoa mchango wake kulingana na uwezo wake, ikiwemo tofali
au mfuko wa saruji.
Kwa mujibu
wa Mnyawama, ukarabati huo utahusisha ujenzi wa uzio kuzunguka ofisi, maboresho
ya jengo lote, pamoja na ujenzi wa ukumbi wa ndani kwa ajili ya vikao. Pia,
kutajengwa ukumbi mwingine katika kiwanja kilichopo nyuma ya ofisi kwa matumizi
mbalimbali ya chama.
Kwa wale
watakaoshindwa kufika katika uzinduzi huo, wamehimizwa kuchangia kupitia namba
ya simu ya MPESA 0764 662 049 yenye jina CHADEMA Kanda ya Serengeti, au kupitia
akaunti ya benki ya CRDB namba 015C765639500, yenye jina hilo hilo.
Mnyawama
amesisitiza kuwa ushiriki wa pamoja wa wanachama na wananchi utasaidia
kufanikisha azma ya kuwa na ofisi bora itakayochochea shughuli za chama katika
kanda hiyo.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment