Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Mpanda,
Joseph Lwamba, amefanya ziara katika Mtaa wa Tulieni, Kata ya Nsemulwa,
Manispaa ya Mpanda Aprili 17, 2026 kwa lengo la kusikiliza, kupokea na kutatua
kero za wananchi.
Katika ziara hiyo, Lwamba alikutana na wakazi wa eneo
hilo na kuwapa nafasi ya kueleza changamoto mbalimbali zinazowakabili, huku
akiahidi kuzifanyia kazi kwa kushirikiana na viongozi wa ngazi husika.
Akizungumza na wananchi, alisisitiza umuhimu wa umoja
na mshikamano katika kujiletea maendeleo, akibainisha kuwa ushirikiano kati ya
wananchi na viongozi ni msingi wa kutatua changamoto za jamii.
Aidha, alitoa wito kwa wananchi kuwa makini katika
masuala ya ununuzi na uuzaji wa viwanja ili kuepuka migogoro ya ardhi, huku
akiwataka viongozi wa mtaa kusimamia kikamilifu majukumu yao kwa uadilifu na
uwajibikaji.
Lwamba pia aliwahimiza wananchi kuendeleza upendo na
amani, pamoja na kuacha woga katika kutetea haki zao kwa kufuata taratibu na
sheria zilizopo.
Katika hatua nyingine, alisisitiza umuhimu wa
kupunguza migogoro ya ardhi katika Mtaa wa Tulieni kwa kushirikiana na mamlaka
husika, huku akihimiza uwajibikaji kwa kila mmoja katika kulinda na kusimamia
rasilimali za maeneo yao.
Ziara hiyo ni sehemu ya juhudi za viongozi wa chama kusogea karibu na wananchi ili kusikiliza na kutatua changamoto zao kwa wakati.
Ndg. Joseph Lwamba, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mpanda na mjumbe wa Kamati ya Siasa wilaya, akisikiliza kero za wananchi wa Mtaa wa Tulieni, Kata ya Nsemulwa, Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda.
Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda na akimwakilisha Katibu wa CCM Wilaya ya Mpanda, Ndg. Musa Ramadhan Mwevi, akishiriki kikamilifu katika mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero za wananchi uliofanyika Mtaa wa Tulieni, Kata ya Nsemulwa, Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda.
Wataalamu mbalimbali wa Kata ya Nsemulwa nao walijumuika katika mkutano wa hadhara uliofanyika Mtaa wa Tulieni, Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda.
Ndg. Kaswiza, mjumbe wa Kamati ya Siasa Wilaya ya Mpanda, akishiriki kikamilifu mkutano wa hadhara uliofanyika Mtaa wa Tulieni, Kata ya Nsemulwa, Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda.
Wananchi wakiwa katika mkutano wa hadhara uliofanyika Mtaa wa Tulieni, Kata ya Nsemulwa, Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda.
Wananchi wakiwa katika mkutano wa hadhara uliofanyika Mtaa wa Tulieni, Kata ya Nsemulwa, Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda.
Wananchi wakiwa katika mkutano wa hadhara uliofanyika Mtaa wa Tulieni, Kata ya Nsemulwa, Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda.
Wananchi wakiwa katika mkutano wa hadhara uliofanyika Mtaa wa Tulieni, Kata ya Nsemulwa, Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda.
Mh. Diwani wa Kata ya Nsemulwa, Ndg. Alex, akisalimia wananchi katika mkutano huo wa hadhara na kuwaomba kudumisha umoja na mshikamano katika kutekeleza majukumu mbalimbali ya maendeleo ya Kata ya Nsemulwa, Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda.
Viongozi wa Kamati ya Siasa kata wakiwa katika mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero mbalimbali za wananchi wa Mtaa wa Tulieni, Kata ya Nsemulwa, Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda.
Wananchi wakiwa katika mkutano wa hadhara uliofanyika Mtaa wa Tulieni, Kata ya Nsemulwa.
Wananchi wakiwa katika mkutano wa hadhara uliofanyika Mtaa wa Tulieni, Kata ya Nsemulwa, Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda.SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment