Na.Mwandishi Wetu
TUME ya Ushindani (FCC) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini imeadhimisha Wiki ya Haki za Mlaji Duniani kwa kutoa msaada wa vifaa tiba katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya, ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za kuboresha huduma za afya kwa wananchi.
Shughuli hiyo imefanyika tarehe 31 Machi, 2026 ambapo FCC imekabidhi vifaa tiba vinne vya Oxygen Flow Meter vitakavyosaidia wagonjwa wanaohitaji huduma ya hewa tiba, hususan wale wanaopata changamoto ya kupumua.
Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano hayo, Mkuu wa FCC Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Bw.Dickson Mbanga, amesema kuwa tukio hilo ni sehemu ya kuadhimisha Wiki ya Haki za Mlaji Duniani pamoja na kutimiza miaka mitatu tangu kuanzishwa kwa ofisi hiyo katika ukanda huo.
Mbanga ameeleza kuwa FCC imeona ni vyema kutumia maadhimisho hayo kwa kutoa mchango wa kijamii utakaoleta tija moja kwa moja kwa wananchi, hasa katika sekta ya afya ambayo ni nyeti na muhimu kwa ustawi wa jamii.
"Vifaa hivyo vitasaidia kuongeza uwezo wa hospitali katika kuhudumia wagonjwa wanaohitaji msaada wa hewa tiba, hivyo kupunguza changamoto zinazoweza kujitokeza wakati wa utoaji wa huduma hizo."amesema Bw.Mbanga
Kwa upande wake, akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya, Muuguzi Kiongozi Ndg. Petro Seme ametoa shukrani za dhati kwa FCC kwa msaada huo muhimu.
Seme amesema kuwa vifaa hivyo ni vya kisasa na vina uwezo wa kuhudumia wagonjwa wawili kwa wakati mmoja, jambo ambalo litarahisisha upatikanaji wa huduma ya hewa tiba na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wagonjwa.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment