" KATIBU WA SENETI SHINYANGA ATOA WITO WA KULINDA AMANI KWA VIJANA WA VYUO

KATIBU WA SENETI SHINYANGA ATOA WITO WA KULINDA AMANI KWA VIJANA WA VYUO

Na Mapuli Kitina Misalaba

Katibu wa Seneti Mkoa wa Shinyanga, Lukomanga Jinyage, amewataka vijana wa vyuo mkoani humo kuthamini na kulinda amani ya nchi, akisisitiza kuwa amani ndiyo msingi wa maendeleo ya taifa na ustawi wa vizazi vijavyo.

Akizungumza na wanachuo wa Chuo cha St. Joseph mjini Shinyanga wakati wa ziara ya Seneti katika vyuo mbalimbali, Jinyage amesema hakuna mtu kutoka nje ya nchi atakayekuja kulinda amani ya Tanzania, hivyo ni wajibu wa kila mwananchi hususan vijana kuhakikisha inalindwa na kudumishwa.

“Tambueni kuwa amani ya nchi yenu ni hazina kubwa sana. Hakuna mtu kutoka nje atakayekuja kuitunza kwa niaba yenu, hivyo ni jukumu letu sote kuhakikisha tunailinda kwa nguvu zote kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho,” amesema Jinyage.

Ameonya kuwa baadhi ya kauli kutoka kwa watu katika jamii, wakiwemo wazee, zinaweza kuwa chanzo cha kuvuruga amani endapo hazitachukuliwa kwa busara, akiwataka vijana kuwa na uelewa mpana na kufanya maamuzi sahihi.

“Wakati mwingine unaweza kusikia ushawishi wa kushiriki vitendo vinavyoweza kuvuruga amani. Ni muhimu vijana mkatumia busara na kujiuliza kama kweli yanayoshauriwa yana manufaa kwa taifa. Kila mmoja ana wajibu wa kulinda amani,” ameongeza.

Aidha, amewasisitiza wanachuo kuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha mshikamano, kuheshimu sheria na kushiriki katika shughuli za maendeleo ili kuhakikisha nchi inaendelea kuwa salama na yenye utulivu.

Ziara ya Seneti Mkoa wa Shinyanga inaendelea katika vyuo mbalimbali, ikiwa na lengo la kutoa elimu, kusikiliza changamoto za wanachuo na kuimarisha uongozi wa wanafunzi katika taasisi za elimu ya juu.

Viongozi wa Seneti Mkoa wa Shinyanga wakizungumza na wanachuo wa St. Joseph, wakitoa elimu kuhusu fursa za ajira, uongozi na masuala ya jamii.Katibu wa Seneti Mkoa wa Shinyanga Lukomanga Jinyage akieleza umuhimu wa kulinda amani na mshikamano kwa maendeleo ya vijana na taifa kwa ujumla.

Katibu Hamasa wa Seneti Mkoa wa Shinyanga Sharon Callist Mathias akihamasisha wanachuo kushiriki kikamilifu katika uongozi na shughuli za maendeleo.



 SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post