" KISA CHA SEHEMU NYETI CHAWAINGIZA MATATANI WATUHUMIWA WAWILI SHINYANGA

KISA CHA SEHEMU NYETI CHAWAINGIZA MATATANI WATUHUMIWA WAWILI SHINYANGA

Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limewakamata watuhumiwa wawili, Kisaka Elinihaki (22) na Makoye James, kwa tuhuma za kusambaza taarifa za uongo kuhusu kupoteza sehemu zao za siri, jambo lililosababisha taharuki kubwa kwa wananchi katika Wilaya ya Kahama.

Taarifa hiyo imetolewa leo, Aprili 7, 2026, na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Janeth Magomi, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.

Kwa mujibu wa Kamanda Magomi, tukio la kwanza lilitokea Aprili 4, 2026 katika Soko Kuu lililopo eneo la Stendi Kuu ya Mabasi, Kata ya Kahama Mjini. Katika tukio hilo, Kisaka Elinihaki, mkazi wa Majengo, alidai kupoteza sehemu zake za siri kimiujiza baada ya kuguswa bega la kushoto na dereva aitwaye Joseph Godfrey (36), mkazi wa Shunu.

Amesema madai hayo ya uongo yalisababisha taharuki kubwa miongoni mwa wananchi waliokuwepo eneo hilo, ambapo baadhi yao walichukua sheria mkononi na kuanza kumshambulia Joseph Godfrey wakimtuhumu kuhusika na tukio hilo.

Hata hivyo, Jeshi la Polisi lilifika kwa wakati na kufanikiwa kumwokoa mtuhumiwa huyo pamoja na kumchukua Kisaka kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Aidha, tukio la pili lilitokea Aprili 6, 2026 katika eneo la machimbo ya dhahabu Mwime, wilayani Kahama, ambapo kijana aitwaye Makoye James alitoa taarifa ya uongo akidai kupoteza sehemu zake za siri baada ya kushikwa na abiria mwenzake alipokuwa akisafiri kwa pikipiki.

Kamanda Magomi ameeleza kuwa tukio hilo pia lilizua taharuki na kusababisha mkusanyiko wa wananchi wenye hasira waliokuwa wakitaka kumshambulia mtu aliyekuwa akituhumiwa, kabla ya polisi kufika na kudhibiti hali hiyo.

Ameongeza kuwa uchunguzi wa kitabibu uliofanyika katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama ulithibitisha kuwa mhusika hakuwa na tatizo lolote, hivyo kuthibitisha kuwa taarifa aliyotoa ilikuwa ya uongo. Mtuhumiwa huyo naye amekamatwa na hatua za kisheria zinaendelea kuchukuliwa dhidi yake.

Kamanda Magomi ameonya kuwa vitendo vya kusambaza taarifa za uongo vina madhara makubwa kwa jamii, ikiwa ni pamoja na kusababisha uvunjifu wa amani, kuwadhuru watu wasio na hatia na hata kuhatarisha maisha.

Ametoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kuzua taarifa zisizo na ukweli na badala yake kushirikiana na vyombo vya dola katika kudumisha amani na usalama.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limeeleza kuwa halitasita kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya mtu yeyote atakayebainika kusambaza taarifa za uongo zinazoweza kuhatarisha usalama wa jamii.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

 
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post