" MANTRA TANZANIA TEYARI KWA TAMASHA LA KIMATAIFA LA NUCLEAR KIDS

MANTRA TANZANIA TEYARI KWA TAMASHA LA KIMATAIFA LA NUCLEAR KIDS

Kampuni ya Mantra Tanzania Limited imeendelea kuonesha dhamira yake thabiti ya kuibua na kukuza vipaji vya watoto nchini kwa kuzindua awamu ya nne ya mchakato wa kusaka na kuwaandaa washiriki wa tamasha la kimataifa la sanaa la watoto wenye umri wa miaka 10 hadi 16 lijulikanalo kama “Nuclear Kids.” Hatua hii ni muendelezo wa mafanikio ya awamu zilizopita, ambapo watoto wa Kitanzania waliweza kushiriki na kuiwakilisha nchi kwa ufanisi mkubwa katika jukwaa la kimataifa.Tamasha la “Nuclear Kids” linaendeshwa na shirika la serikali ya Urusi, Rosatom, likiwa na lengo la kuwaleta pamoja watoto wenye vipaji kutoka familia zinazohusiana na sekta ya nishati ya nyuklia pamoja na nchi washirika. Kupitia jukwaa hili, washiriki hupata nafasi ya kushiriki katika maandalizi ya onesho kubwa la muziki linalojumuisha uimbaji, uigizaji na uchezaji, huku likiwa na ubunifu wa hali ya juu unaovutia hadhira ya kimataifa.Kwa upande wa Tanzania, ushiriki katika tamasha hili umeendelea kuwa chachu ya maendeleo kwa watoto wengi wenye vipaji mbalimbali vya sanaa. Mafunzo wanayopatiwa kabla na wakati wa tamasha huwasaidia kukuza nidhamu ya kazi, kujiamini wanapokuwa jukwaani, pamoja na kujenga uwezo wa kufanya kazi kwa ushirikiano na wenzao kutoka tamaduni tofauti.Mbali na kukuza vipaji, mradi huu pia unalenga kuimarisha mshikamano na urafiki miongoni mwa watoto kutoka mataifa mbalimbali. Kupitia sanaa, washiriki hubadilishana tamaduni, kujifunza mitazamo mipya na kujenga mahusiano ya kudumu yanayovuka mipaka ya nchi zao, jambo linalochangia kukuza kizazi chenye mtazamo mpana wa kimataifa.Kwa ujumla, “Nuclear Kids” imeendelea kuwa jukwaa muhimu la kukuza vipaji vya watoto, kutoa elimu kupitia sanaa na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa. Juhudi za Mantra Tanzania Limited zinastahili pongezi kwa mchango wake katika kuwajengea watoto uwezo wa kisanaa na kuitangaza Tanzania kimataifa kupitia ubunifu na vipaji vyao.


 SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

 
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post