" MIGOGORO YA KIFAMILIA YACHANGIA ONGEZEKO WATOTO WA MITAANI

MIGOGORO YA KIFAMILIA YACHANGIA ONGEZEKO WATOTO WA MITAANI

Na, Egidia Vedasto,

Misalaba Media, Arusha.

Idadi ya watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani imezidi kuongezeka siku hadi siku sababu ikitajwa kuwa ni kukithiri kwa migogoro ya kifamilia.

Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya mtoto anayeishi na kufanya kazi mitaani Mratibu wa Shirika la Amani lililopo Kata ya Kaloleni Jijini Arusha linalofanya kazi ya kuokoa na kuwaweka mazingira salama watoto wanaoishi mitaani na wale wanaopitia ukatili, Naomi Kimaro amesema tangu January hadi March mwaka huu jumla ya watoto 42 wameokolewa.

Aidha amesema watoto wengi wanapohojiwa sababu inayowafanya wakimbie kwa wazazi wao na kuishi mitaani wanataja  ugomvi wa wazazi na migogoro ya kifamilia, na wachache wao wakitaja ugumu wa maisha unaohusishwa na masuala ya rika.

"Naiasa jamii tushirikiane kwa pamoja kuwaokoa watoto wanaoishi mitaani, tutoe taarifa pale mtoto akionekana hayuko katika mazingira salama, mtoto kupigwa kupita kiasi wanaobakwa na kurawitiwa. Viongozi wa dini zungumzeni na waumini wenu na kuiasa jamii iwe na utaratibu wa kusuruhisha matatizo bila kuathiri watoto, naamini tukishirikiana kwa pamoja tutapunguza ongezeko hili" amesema Naomi.

Kwa upande wake Khatib Kasim (17) aliyeokolewa na Shirika la Amani amesema sababu iliyomfanya kukimbilia mtaani ni kushindwa kuishi na baba yake mzazi baada ya ndoa ya wazazi wake kuvunjika.

"Kwa sasa natengeneza (culture) urembo, Shirika liliniokoa miaka nane iliyopita limenilea na sasa nimepata ujuzi nafanya shughuli zangu, pia Shirika lina mpango wa kuniunganisha na wafanya biashara wakubwa wa culture wenye uhakika wa masoko ili kuniongezea kipato",

"Ugomvi ulipozidi mama aliondoka kurudi kwao,  baba alizidisha ulevi hivyo nikashindwa kuishi nyumbani, niliondoka kuelekea mtaani na bahati nzuri nikaokolewa na Shirika la Amani, wito wangu kwa wazazi wote wajifunze kuishi vizuri na kumaliza migogoro yao na kulea watoto wao pamoja, wazazi wakitofautiana anayeumia ni mtoto" ameeleza Khatib.

Shirika la Amani Katika kuadhimisha siku ya mtoto anayeishi na kufanya kazi mitaani Duniani limetimiza miaka 25 likifanya kazi ya kuokoa na kulea, kutoa ushauri nasihi na kuwaunganisha watoto na familia zao, kuhakikisha wanaendelea na masomo na kutimiza ndoto zao.  

Hata hivyo mafanikio ambayo Shirika linajivunia ni kuona watoto wengi  waliokuwa mitaani  wakifanikiwa kuwa Wahandisi, Wahasibu, Walimu na wengine kutimiza ndoto za kujisimamia wenyewe. Maadhimisho ya mwaka huu yamebeba kaulimbiu "Malezi na Ulinzi wa Wtoto Wanaoishi na Kufanya Kazi  Mitaani ni Wajibu Wetu Sote".

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

 
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post