Na Mapuli Kitina Misalaba
Mzunguko wa pili wa marudiano wa mashindano ya
NIACHEKONA CUP 2026 umeanza rasmi leo Jumatano Mei 27, 2026 kwa mchezo wa
ushindani mkubwa uliochezwa katika uwanja wa Mwabenda kata ya Solwa,
Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ambapo timu ya HOME BOYS imeibuka na ushindi
wa bao 1-0 dhidi ya MANHEIGANA FC.
Kutokana na matokeo hayo, timu ya MANHEIGANA FC
imeondolewa rasmi kwenye mashindano hayo baada ya kupoteza pointi muhimu katika
mchezo wa leo.
Ikumbukwe kuwa timu hizo mbili ndiyo zilizofungua
rasmi mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 ambapo katika mchezo wa ufunguzi
zilitoshana nguvu kwa sare ya bao 1-1 kabla ya HOME BOYS kuibuka na ushindi
katika mchezo wa leo wa marudiano.
Mashabiki wa HOME BOYS wameendelea kuonesha furaha na
matumaini makubwa kufuatia ujio wa kocha mpya wa timu hiyo baada ya kuachana na
kocha wa awali, huku wakiamini mabadiliko hayo yataisaidia timu yao kufanya
vizuri zaidi katika mashindano hayo.
Akizungumza baada ya ushindi huo, kocha mpya wa HOME
BOYS amesema malengo yake makubwa ni kuhakikisha timu hiyo inafika hatua ya
fainali na hatimaye kutwaa ubingwa wa NIACHEKONA CUP 2026.
Kwa upande wao viongozi wa MANHEIGANA FC wamemshukuru
mwandaaji wa mashindano hayo Bwana Paul Daud Augustino kwa kuwapa nafasi ya
kushiriki katika mashindano hayo huku wakisema wamejifunza mambo mengi kupitia
ushindani walioupata ndani ya ligi hiyo.
Aidha baada ya kuondolewa katika mashindano hayo, timu
hiyo imeomba kupewa nafasi ya Mshindwa bora (Best Rooza) kutokana na namna
walivyopambana na kushiriki kwa ushindani katika michezo yao yote.
Baada ya mchezo huo, Katibu wa Kamati ya Mashindano
Sambayi Jilya ametangaza ratiba ya mchezo wa kesho ambapo timu ya MWASENGE FC
kutoka kata ya Salawe itamenyana na UFUKUNYUNGU FC kutoka kata ya Ngokolo mjini
Shinyanga katika mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Sambayi ameendelea kuwahimiza wananchi pamoja na
mashabiki wa timu hizo kujitokeza kwa wingi katika uwanja wa Mwabenda
kushuhudia burudani ya soka pamoja na vipaji vya vijana vinavyoendelea
kuonekana kupitia mashindano hayo.
Mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 yameandaliwa na
Bwana Paul Daud Augustino kupitia ufadhili wa shirika la Lushu Foundation kwa
lengo la kuibua vipaji vya vijana, kukuza michezo pamoja na kuimarisha
mshikamano wa jamii kupitia soka.
Kwa huduma za ushereheshaji wa shughuli mbalimbali,
matangazo pamoja na burudani unaweza kuwasiliana na MC NIACHEKONA kupitia namba
0757 267 738.
Timu ya MANHEIGANA FC.
Wachezaji wa HOME BOYS na MANHEIGANA FC wakioneshana ushindani mkubwa katika mchezo wa mzunguko wa pili wa NIACHEKONA CUP 2026 uliochezwa uwanja wa Mwabenda kata ya Solwa leo Mei 27, 2026.
Wachezaji wa HOME BOYS na MANHEIGANA FC wakioneshana ushindani mkubwa katika mchezo wa mzunguko wa pili wa NIACHEKONA CUP 2026 uliochezwa uwanja wa Mwabenda kata ya Solwa leo Mei 27, 2026.
Mchezo ukiendelea ambapo HOME BOYS iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya MANHEIGANA FC katika pambano lililovutia mashabiki wengi.
Mashabiki wa soka wakifuatilia kwa hamasa kubwa mchezo wa HOME BOYS dhidi ya MANHEIGANA FC uliomalizika kwa ushindi wa bao 1-0.

Viongozi pamoja na wadau wa michezo wakifuatilia mchezo wa mzunguko wa pili wa NIACHEKONA CUP 2026 katika uwanja wa Mwabenda.
Mchezo ukiendelea ambapo HOME BOYS iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya MANHEIGANA FC katika pambano lililovutia mashabiki wengi.
Mashabiki na wananchi wakifuatilia burudani ya soka kupitia mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 leo Mei 27, 2026 katika uwanja wa Mwabenda kata ya Solwa.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment