" Mke wa Trump Akanusha Kuwa na Uhusiano na Epstein Baada ya Nyaraka Kuibuka

Mke wa Trump Akanusha Kuwa na Uhusiano na Epstein Baada ya Nyaraka Kuibuka

 


Mke wa Rais wa Marekani, Melania Trump usiku wa kuamkia leo Aprili 10, 2026 amekanusha vikali madai yanayomhusisha na mfanyabiashara marehemu Jeffrey Epstein pamoja na mshirika wake Ghislaine Maxwell, akiyaita madai hayo kuwa ni taarifa ya uongo na watu wanataka kumchafua.

Kauli hiyo imekuja baada ya kuibuka kwa nyaraka zilizotolewa na U.S. Department of Justice, zikionyesha mawasiliano ya barua pepe ya mwaka 2002 kati ya mtu anayejiita “Melania” na mtu anayedhaniwa kuwa Maxwell.

Katika barua pepe hiyo, Melania anaonekana kumwandikia Maxwell kwa lugha ya kirafiki akimpongeza kwa picha yake iliyochapishwa kwenye jarida na kumtaja Epstein kwa kifupi kama “JE.” Pia anaeleza nia ya kukutana naye pindi atakaporejea New York.

Hata hivyo, katika majibu ya mwaka 2003, mtu anayetambulika kama “G. Max” alimjibu akisema ana ratiba yenye shughuli nyingi na huenda asipate muda wa kukutana.

Pamoja na kuibuka kwa mawasiliano hayo, Melania Trump amesisitiza kuwa hakuwahi kuwa na urafiki wala uhusiano wa karibu na Epstein au Maxwell. Amesema barua pepe hiyo ilikuwa ni mawasiliano ya kawaida tu yasiyo na uzito wowote.

“Jibu langu la barua pepe haliwezi kutafsiriwa kama kitu zaidi ya mawasiliano ya kawaida,” amesema.

Aidha, Melania ameeleza kuwa hajawahi kusafiri kwa ndege binafsi ya Epstein wala kutembelea kisiwa chake, huku akisisitiza kuwa hakuwahi kuwa na ufahamu wowote kuhusu vitendo vya unyanyasaji vilivyohusishwa naye.

Picha moja ya zamani inayowaonyesha Melania, mumewe Donald Trump, Epstein na Maxwell wakiwa pamoja katika hafla ya kijamii imekuwa ikisambaa mitandaoni, jambo lililochochea mjadala zaidi.

Hata hivyo, wachambuzi wa masuala ya sheria na siasa wanasema kuwa hadi sasa, ushahidi uliopo unaonyesha uwepo wa mawasiliano ya kijamii tu, bila kuthibitisha uhusiano wa karibu au kuhusika kwa namna yoyote katika vitendo vya uhalifu.

Melania Trump pia ametoa wito kwa mamlaka kuendelea kuweka wazi ukweli wote kuhusu sakata la Epstein ili haki itendeke kwa waathirika wote.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

 
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post