" MNEC NDELE AVUTIWA NA SAUTI YA MRENO ATAMANI ANGEKUWA BBC KIUTANGAZAJI

MNEC NDELE AVUTIWA NA SAUTI YA MRENO ATAMANI ANGEKUWA BBC KIUTANGAZAJI


Na Lydia Lugakila, Misalaba MediaMbeyaMjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Ndele Mwaselela, ameonesha kuvutiwa kwa kiwango kikubwa na kipaji cha kijana Suleiman Mreno kutoka Taasisi ya Turia Trust, kitengo cha Habari na Mawasiliano, akitaja sauti yake kuwa ya kipekee, yenye mvuto na isiyochosha kusikilizwa.Ndele alitoa kauli hiyo leo Aprili 22, 2026, wakati wa uzinduzi wa kituo cha habari mkoani Mbeya kinachomilikiwa na mkongwe wa tasnia ya habari, Ezekiel Kamanga.Akizungumza katika hafla hiyo, Ndele alisema anatamani kumuona Suleiman Mreno akifikia hatua ya kuwa mtangazaji wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), akisisitiza kuwa ana uwezo mkubwa na kipaji cha nadra kinachostahili kuendelezwa katika viwango vya kimataifa.Kauli hiyo ya Ndele imekuja baada ya Kijana Suleiman Mreno kutoa neno la kumpongeza Ezekiel Kamanga mkongwe wa habari Mkoani Mbeya ambapo amempongeza kwa namna alivyoshirikiana na vyombo vingi vya habari Mkoani Mbeya na nje ya Mkoa huo kuhabarisha jamii.“Kwa kweli huyu kijana ana sauti ya kipekee sana ni sauti ambayo haichoshi kusikiliza, na naamini anaweza kufanya vizuri hata kwenye majukwaa makubwa ya kimataifa kama BBC,” alisema Ndele.Kiongozi huyo ametumia nafasi hiyo kuwasihi waandishi wa habari kuona ni namna gani wataibua vipaji vyao kwa kukaa pamoja na kuongeza kuwa yeye yuko tayari kushirikiana na wanahabari au mwanahabari atakayeonesha ubunifu, kujituma na kupambana katika maisha.Mbali na hilo, Ndele alimpongeza Ezekiel Kamanga kwa uwekezaji wake katika sekta ya habari kwa kuzindua kituo hicho, akionesha kumuunga mkono kwa vitendo kwa kumpatia msaada wa vifaa muhimu ikiwemo kamera na kompyuta mpakato (laptop) ili kurahisisha shughuli za uandishi wa habari.Akitaja dhamira ya kuanzisha kituo hicho, Kamanga amesema lengo ni kupanua upatikanaji wa habari sahihi na kwa wakati kwa wananchi, kuibua na kutangaza fursa mbalimbali za maendeleo zilizopo mkoani Mbeya, pamoja na kutoa jukwaa la kuelimisha na kuhamasisha jamii kushiriki kikamilifu katika masuala ya kijamii na kiuchumi.Aidha,Kamanga  aliwapongeza waandishi wa habari wenzake kwa mchango wao mkubwa katika kuhabarisha umma na kusisitiza kuendelea kushirikiana kuinua tasnia ya habari nchini huku akiwashukuru waandishi hao waliomuunga mkono katika kazi hiyo ambapo pia  amejivunia kuzalisha vijana wengi kupitia tasnia hiyo waliopita mkononi mwake.Kijana Suleiman Mreno kutoka Taasisi ya Turia Trust mwenye sauti ya kipekee aliyemvutia Mnec Ndele Mkoani Mbeya

 SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post