
Moto mkubwa umezuka Aprili 4, 2026 katika eneo la Ubungo, karibu na kituo cha mabasi cha Mawasiliano, na kusababisha uharibifu wa mali baada ya kuteketeza maduka na vibanda vya wafanyabiashara wadogo.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, moto huo ulianza ghafla na kuenea kwa kasi katika eneo hilo, huku chanzo chake kikiwa bado hakijafahamika hadi sasa.
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limefika eneo la tukio na linaendelea na jitihada za kuudhibiti moto huo, likisaidiwa na wananchi waliokuwepo jirani.
Hakuna taarifa rasmi iliyotolewa kuhusu idadi ya majeruhi au hasara kamili iliyosababishwa na moto huo, huku mamlaka zikiahidi kutoa taarifa zaidi pindi uchunguzi utakapokamilika.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment