" Muhoozi aipa siku saba Iran kuomba radhi kwa Uganda

Muhoozi aipa siku saba Iran kuomba radhi kwa Uganda

 

Muhoozi aipa siku saba Iran kuomba radhi kwa Uganda

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Uganda (UPDF), Muhoozi Kainerugaba, amezua mjadala mkali kimataifa baada ya kutoa kauli kali dhidi ya Iran kupitia ukurasa wake wa X Aprili 2, 2026.

 

Katika ujumbe huo, Jenerali Muhoozi ametoa onyo la moja kwa moja kwa Iran akilitaka taifa hilo kuomba radhi kwa Uganda ndani ya siku saba. Kauli hiyo imeibua maswali kuhusu mustakabali wa uhusiano wa kidiplomasia kati ya mataifa hayo mawili.

Aidha, Muhoozi amedai kuwa hakuna taifa lolote duniani lenye uwezo wa kuishinda UPDF kijeshi, kauli iliyozidi kuchochea mjadala katika medani za kimataifa.

Mbali na hilo, ameeleza kuwa vyombo vya usalama vya Uganda vinawashikilia watu aliowataja kuwa ni wapelelezi wa Iran waliokuwa wakifanya shughuli nchini humo, ingawa hakutoa maelezo ya kina kuhusu mazingira ya kukamatwa kwao wala ushahidi wa madai hayo.

Kauli hizo zimeendelea kuzua hisia tofauti huku wachambuzi wa siasa wakitathmini athari zake kwa uhusiano wa kimataifa na usalama wa kikanda

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

 
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post