
Mkuu wa Majeshi wa Uganda, Jenerali Muhoozi Kainerugaba, amezua mjadala mkubwa kimataifa baada ya kuchapisha jumbe mbili zenye utata kwenye mtandao wa X ndani ya saa chache.
Katika ujumbe wake wa kwanza, alitangaza kuwa yuko tayari kupeleka wanajeshi 100,000 wa Uganda kwenda kuilinda Israel, akisisitiza kuwa ni “Nchi Takatifu, nchi ya Yesu Kristo Mungu wetu.” Kauli hiyo imeibua hisia mseto kutokana na uzito wake kisiasa na kidini.
Baadaye, Jenerali Kainerugaba alichapisha ujumbe mwingine mkali zaidi, akidai kuwa ana takribani vijana 500,000 “wenye njaa ya vita” walio tayari kuivamia Tehran bila malipo. Kauli hii imeonekana kuwa ya uchokozi na imezua mjadala mpana kuhusu msimamo wa Uganda katika masuala ya kimataifa, hasa katika mivutano ya Mashariki ya Kati.
Si mara ya kwanza kwa Jenerali Kainerugaba kutoa matamshi ya aina hii. Mwezi Machi 2026, aliweka wazi uungaji mkono wake kwa Israel, akisema kuwa jaribio lolote la kuiangamiza au kuishinda nchi hiyo lingeifanya Uganda iingie vitani upande wa Israel.
Akiwa Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Uganda (UPDF), amezoeleka kwa kauli zake za moja kwa moja na zenye kuvuta hisia kwenye mitandao ya kijamii, hasa kuhusu masuala ya kimataifa.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment