" Rais Samia apunguza idadi magari katika misafara yake

Rais Samia apunguza idadi magari katika misafara yake

 

Rais Samia apunguza idadi magari katika misafara yake

RAIS Samia Suluhu Hassan, ametangaza kupunguza idadi ya magari kwenye misafara yake mbalimbali ya kikazi ikiwa ni moja ya mkakati wa kupunguza matumizi makubwa ya mafuta serikalini.

Samia, amesema hayo leo Ikulu ya Chamwino, baada ya kuwaapisha viongozi mbalimbali wa serikali aliowateuwa kushika nafasi mbalimbali hivi karibuni.

Amesema, serikali imekuwa mtumiaji mkubwa wa mafuta hivyo kupanda kwa bei hakuna budi kupunguza kwa kiasi kikubwa matumizi hayo.

“Wakati wa msiba wa Lukuvi, nilisema kidogo leo naomba nitumia fursa hii kuzungumza kuhusu hali ya dunia ilivyo sasa hali tumeiona imeleta athari kwa ulimwengu mzima, wiki iliyopita nilikuwa naangalia bei za mafuta kwa nchi mbalimbali ulimwenguni nikaona kwa Ulaya ni Euro 600 na Marekani Dola 800,” amesema.
Amesema, wakati nchi za Ulaya na Marekani hali ikiwa hivyo huku Afrika mambo yako juu zaidi, ambapo baadhi ya nchi zimefikia hatua ya kutoa ruhusa kwa watu kufanyia kazi nyumbani ili kuondoa matumizi ya magari kwenda kazini na kurudu nyumbani.

“Kuna nchi tayari ambazo zimeshawapa watu ruhusa ya kufanya kazi majumbani kusiwe na matumizi ya magari kwenda maofisini na kurudi, lakini kuna nchi ambazo kwa kiasi kikubwa zimepunguza matumizi ya mafuta na wanaupungufu wa mafuta.

“Leo tumeamka na neno la faraja kwamba angalau pale Hormuz angalau ukiongea nao vizuri wale jamaa vimeli vinapitapita kwahiyo inatupa matumani kwamba meli itapita,” amesema Rais Samia

 
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post