" JESHI LA POLISI SHINYANGA LAKAMATA WAHALIFU 35

JESHI LA POLISI SHINYANGA LAKAMATA WAHALIFU 35

Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limefanikiwa kukamata jumla ya watuhumiwa 35 wanaodaiwa kujihusisha na vitendo vya uhalifu katika operesheni zilizofanyika kuanzia Machi 1 hadi Machi 31, 2026.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), kukamatwa kwa watuhumiwa hao kunahusishwa na operesheni maalum zilizofanyika katika maeneo ya mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR katika wilaya za Msalala na Shinyanga.

Katika operesheni hizo, Polisi wamefanikiwa kukamata vielelezo mbalimbali vikiwemo pinde 306, nondo, mabomba 32 ya ukubwa wa mm12, stendi za makarasha 12 pamoja na mabomba ya mraba (square pipe) 65.

Aidha, kwa upande wa usalama barabarani, Jeshi la Polisi kupitia Kikosi cha Usalama Barabarani limeendesha operesheni dhidi ya madereva wanaokiuka sheria, ambapo madereva wawili walifungiwa leseni zao kwa kipindi cha miezi mitatu baada ya kubainika kuendesha gari kwa mwendo kasi zaidi ya kilomita 80 kwa saa (80KPH).

Katika ukaguzi huo, jumla ya makosa 5,648 ya barabarani yalibainika, ambapo makosa ya magari yalikuwa 4,044 na yale ya bajaji na pikipiki yalifikia 1,604, huku wahusika wakitozwa faini papo kwa papo.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga linatoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama kwa kutoa taarifa za uhalifu, sambamba na kuwakumbusha wazazi na walezi kuongeza uangalizi kwa watoto katika kipindi hiki cha Sikukuu za Pasaka.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

 
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post