Na Mapuli Kitina Misalaba
Katika kuadhimisha Siku ya Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar, Taasisi ya Joseph Muhunda Nyerere Foundation leo Aprili 26, 2026
imeendesha zoezi la upandaji miti katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa
Shinyanga, ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha utunzaji wa mazingira na kuenzi umoja
wa kitaifa.
Akizungumza wakati wa tukio hilo, Mkurugenzi wa
Taasisi hiyo, Joseph Muhunda Nyerere, amesema kuwa maadhimisho ya Muungano
yanapaswa kwenda sambamba na vitendo vinavyogusa maisha ya wananchi, ikiwemo
kulinda mazingira kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
Ameeleza kuwa upandaji miti ni njia mojawapo ya
kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi na kuboresha afya ya
jamii.
Kwa upande wake, Mratibu wa Taasisi hiyo katika
Manispaa ya Shinyanga, Mwalimu Leonard Mapolu, amesema taasisi hiyo imekuwa
mstari wa mbele katika kuendesha kampeni za mazingira, hususan upandaji miti,
na kwamba wataendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha mji wa
Shinyanga unakuwa wa kijani na salama kiafya.
Naye Mratibu mwingine wa Taasisi hiyo, Abdalah Sube,
amesisitiza umuhimu wa jamii kushiriki kikamilifu katika uhifadhi wa mazingira,
akibainisha kuwa juhudi za pamoja ndizo zitakazosaidia kufikia malengo ya
maendeleo endelevu.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa
Shinyanga, Dkt. Luzila John, ameishukuru taasisi hiyo kwa kuchagua hospitali
hiyo kama eneo la zoezi hilo, akieleza kuwa miti hiyo itasaidia kuboresha
mazingira ya hospitali na kutoa hewa safi kwa wagonjwa na watumishi wa afya.
Dkt. Luzila pia alishiriki kikamilifu katika zoezi la upandaji miti.
Aidha, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Manispaa ya
Shinyanga, ambaye alikuwa miongoni mwa mashuhuda wa Muungano, alitoa simulizi
ya kihistoria akieleza kuwa wakati Muungano unapatikana alikuwa na umri wa
takribani miaka 10 ambapo amesema amani iliyojengwa tangu wakati huo imekuwa
nguzo muhimu ya kuudumisha Muungano na maendeleo ya Taifa.
Taasisi ya Joseph Muhunda Nyerere Foundation
imeendelea kujikita katika masuala ya uhifadhi wa mazingira nchini, ikiwa ni
pamoja na kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii.
Zoezi la upandaji miti limekuwa ni miongoni mwa vipaumbele vyake, hasa katika Manispaa ya Shinyanga, likilenga kuongeza uelewa na kuwahamasisha wananchi kushiriki katika utunzaji wa mazingira.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Joseph Muhunda Nyerere Foundation, Joseph Muhunda Nyerere akizungumza na viongozi na watumishi wa hospitali kabla ya zoezi la upandaji miti, akieleza dhamira ya taasisi katika kuhamasisha utunzaji wa mazingira na kuenzi Siku ya Muungano kwa vitendo.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Luzila John akizungumza na uongozi wa Taasisi ya Joseph Muhunda Nyerere Foundation kabla ya kuanza zoezi la upandaji miti, akisisitiza umuhimu wa kuboresha mazingira ya hospitali kwa afya ya wagonjwa na watumishi.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Luzila John akizungumza na uongozi wa Taasisi ya Joseph Muhunda Nyerere Foundation kabla ya kuanza zoezi la upandaji miti, akisisitiza umuhimu wa kuboresha mazingira ya hospitali kwa afya ya wagonjwa na watumishi.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Joseph Muhunda Nyerere Foundation, Joseph Muhunda Nyerere akipanda mti ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya Muungano kwa vitendo.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Joseph Muhunda Nyerere Foundation, Joseph Muhunda Nyerere akipanda mti ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya Muungano kwa vitendo.
Mratibu wa Taasisi Manispaa ya Shinyanga, Mwalimu Leonard Mapolu akishiriki zoezi la upandaji miti katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Manispaa ya Shinyanga akishiriki kupanda mti kama ishara ya kudumisha amani na Muungano.
Mratibu wa Taasisi, Abdalah Sube akipanda mti kuonesha mfano wa vitendo katika uhifadhi wa mazingira.
Zoezi la upandaji miti likiendelea.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Joseph Muhunda Nyerere Foundation, Joseph Muhunda Nyerere akizungumza kuhusu umuhimu wa utunzaji wa mazingira wakati wa maadhimisho ya Siku ya Muungano.
Mratibu wa Taasisi hiyo Manispaa ya Shinyanga, Mwalimu Leonard Mapolu akielezea juhudi za taasisi katika kuhamasisha upandaji miti kwa maendeleo endelevu.
Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Manispaa ya Shinyanga akitoa ushuhuda wa historia ya Muungano na kusisitiza umuhimu wa amani kwa maendeleo ya Taifa.
Mratibu wa Taasisi, Abdalah Sube akizungumza kuhusu umuhimu wa ushirikiano wa jamii katika kulinda mazingira.SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254























Post a Comment