Wadau wa siasa na wananchi nchini wameupokea uteuzi wa hivi karibuni uliofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan kama hatua madhubuti ya kuimarisha maridhiano ya kitaifa na siasa jumuishi.
Hatua ya Rais kumteua Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Dk. Eveline Munisi kuwa Mbunge, na kumrejesha Profesa Palamagamba Kabudi katika Baraza la Mawaziri, imetajwa kuwa ni ukomavu wa kisiasa unaolenga kuvunja kuta za uadui na kujenga daraja la ushirikiano kwa maslahi mapana ya nchi.
Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, Haji Khamis, amebainisha kuwa uteuzi wa Dk. Munisi ni ishara tosha kuwa siasa si uadui bali ni ushindani wa mawazo kwa ajili ya maendeleo.
Wadau wengine, akiwemo Handhal Al Khaify na Cadillac Frank, wamempongeza Rais kwa kumteua Profesa Kabudi kuongoza Wizara ya Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), wakimtaja kama kiongozi mwenye uzoefu na misimamo inayohitajika katika kusimamia majukumu mazito ya serikali yaliyoachwa na marehemu William Lukuvi.
Pamoja na pongezi hizo, wananchi wamewatwika mzigo wa majukumu viongozi hao wapya wakitaka watekeleze wajibu wao kwa weledi na uadilifu wa hali ya juu. Wito umetolewa kwa wateule hao kuweka mbele maslahi ya taifa badala ya binafsi, huku wakitakiwa kuonesha utendaji wenye tija utakaogusa maisha ya wananchi wa kawaida, hususan katika kipindi hiki ambacho taifa linajikita katika utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya 2050.
Kwa upande mwingine, taasisi ya Women in Leadership Forum (WLF) imeutaja uteuzi huo kama ushindi kwa wanawake wanaochipukia katika uongozi wenye maono.
Wakati Profesa Kabudi akiahidi kulitumikia taifa kwa juhudi na uaminifu, mabadiliko haya ya safu yanatajwa kuwa ni sehemu ya mageuzi ya kimkakati ya Rais Samia katika kuhakikisha taasisi za umma, ikiwemo EWURA, zinaongozwa na viongozi wenye uwezo wa kuendana na kasi ya mabadiliko ya kiuchumi na kijamii nchini Tanzania.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment