Na Tonny Alphonce-Misalaba MediaVijana mkoani Mwanza wameipongeza Serikali kupitia Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana kufuatia hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2026/2027 iliyowasilishwa bungeni wiki hii, wakieleza kuwa inaonesha dhamira ya dhati ya kumkomboa kijana kiuchumi.Pongezi hizo zimekuja mara baada ya Waziri, Dkt. Joel Nanauka, kuwasilisha bajeti inayolenga kuimarisha uwezeshaji wa vijana, kundi ambalo linaendelea kuwa mhimili mkubwa wa nguvu kazi ya Taifa.Akizungumza na blog hii, Bahati Gondwe amesema mipango iliyowekwa awamu hii inaonesha mwelekeo sahihi wa Serikali katika kuwainua vijana kiuchumi kupitia uwezeshaji na fursa za kujiajiri.“Tunachokiona sasa ni jitihada za makusudi za Serikali kuhakikisha vijana wanapata mitaji, mafunzo na fursa za kiuchumi. Hii ni hatua muhimu sana kwa maendeleo yetu,” amesema Gondwe.Nae mwenyekiti wa waendesha bajaji za Mizigo Willyberth Joseph ambae ni mnufaika amewataka vijana kuhakikisha wanaandaa vitu vyote vinavyohitajika Ili wasikose sifa ya kupata mikopo hiyo.Kwa upande wake, mchambuzi wa masuala ya kijamii na kiuchumi, Hamisi Juma amesema bajeti hiyo imekuja wakati muafaka ambapo vijana wengi wanahitaji msaada wa kimfumo ili kushiriki kikamilifu katika uchumi wa Taifa.“Serikali imeonesha nia njema kwa kuweka mikakati inayolenga kukuza ajira, ubunifu wa kidijitali na upatikanaji wa mitaji. Hata hivyo, changamoto kubwa ipo kwenye utekelezaji,” amesema Juma.Katika hotuba hiyo, Waziri Nanauka alisisitiza umuhimu wa kuwekeza kwa vijana kutokana na idadi yao kubwa nchini, akibainisha kuwa kundi hilo lina nafasi muhimu katika kuchochea ukuaji wa uchumi jumuishi.Aidha, vijana wa Mwanza wameeleza kuwa mikakati ya Serikali katika kukuza ajira na kuimarisha mifuko ya maendeleo ya vijana itasaidia kupunguza changamoto ya ukosefu wa ajira, endapo utekelezaji wake utasimamiwa kwa ufanisi.Wameshauri kuwa ni muhimu kuhakikisha kuwa fursa zinazotolewa zinawafikia vijana wa maeneo yote, hususan walioko vijijini na pembezoni, ili kuhakikisha hakuna anayebaki nyuma katika safari ya maendeleo.Kwa ujumla, matarajio ya vijana wengi nchini ni kuona mipango iliyowasilishwa bungeni inatekelezwa kwa vitendo na kuleta mabadiliko chanya katika maisha yao ya kila siku.SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment