" WANANCHI SHINYANGA WASISITIZA UMUHIMU WA AMANI KATIKA MAISHA YA KILA SIKU

WANANCHI SHINYANGA WASISITIZA UMUHIMU WA AMANI KATIKA MAISHA YA KILA SIKU

Na Mapuli Kitina Misalaba

Baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Shinyanga wamezungumzia umuhimu wa kudumisha amani katika maisha ya kila siku, wakisema kuwa amani ni msingi wa maendeleo ya mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla.

Akizungumza na Misalaba Media, Mkazi wa Mtaa wa Miti Mirefu, Kata ya Mjini, Mzee Ndulu Mipawa amesema kuwa bila amani hakuna shughuli za maendeleo zinazoweza kufanyika kwa ufanisi, akiwahimiza wananchi kuendelea kulinda utulivu uliopo.

Kwa upande wake, Mkazi wa Kata ya Kitangili, Bwana Philipo Maganga Machiya, amesema kuwa amani huleta mshikamano miongoni mwa watu na kusaidia kujenga mahusiano mazuri ndani ya jamii, hali inayochochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Naye Rebeka Godfury, mkazi wa Kata ya Mjini, ameeleza kuwa amani inapaswa kuanzia ngazi ya familia, akisisitiza kuwa maadili mema na kuheshimiana ni nguzo muhimu katika kuimarisha utulivu wa jamii.

Aidha, Mkazi wa Nguzonane, Farda Ntauma, amesema kuwa vijana wanapaswa kuelimishwa juu ya umuhimu wa amani ili kuepuka vitendo vinavyoweza kuhatarisha usalama, akiongeza kuwa jamii yenye amani huwavutia wawekezaji na kuongeza fursa za ajira.

Kwa pamoja, wananchi hao wamewataka Watanzania kuendelea kudumisha mshikamano, kuheshimu sheria na mamlaka zilizopo ili kuhakikisha amani inaendelea kuwepo na kuwa chachu ya maendeleo endelevu.

Mzee Ndulu Mipawa



Post a Comment

Previous Post Next Post