Na Mapuli Kitina Misalaba
Wakazi wawili wa Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga
wamehukumiwa vifungo vya jela baada ya kupatikana na hatia ya kusambaza taarifa
za uongo zilizozua taharuki katika jamii.
Akizungumza na vyombo vya habari leo Aprili 9, 2026,
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, SACP Janeth Magomi, amewataja
waliohukumiwa kuwa ni Kisaka Elininhaki (22), mfanyabiashara, na Makoye James
(20), dereva.
Kwa mujibu wa Kamanda Magomi, wawili hao walikamatwa
kufuatia kusambaza taarifa zisizo za kweli wakidai kupotea kwa sehemu nyeti
kimujiza baada ya kuguswa, hali iliyosababisha hofu na taharuki kwa wananchi.
Ameeleza kuwa baada ya kufikishwa katika Mahakama ya
Wilaya ya Kahama, walipatikana na hatia ya kusambaza taarifa za uongo.
Katika hukumu hiyo, Kisaka Elininhaki amehukumiwa
kifungo cha miezi sita jela, huku Makoye James akihukumiwa kifungo cha miezi
mitano jela.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limewakumbusha
wananchi kuwa kusambaza taarifa za uongo ni kosa la jinai linaloweza
kusababisha madhara makubwa kwa jamii, likiwemo uvunjifu wa amani.
Aidha, wananchi wametakiwa kutoa taarifa sahihi na
kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama ili kudumisha amani na utulivu.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment