Mwenyekiti mstaafu wa Chama cha ADC, Hamad Rashid Mohamed, ameimwagia sifa Tume ya Uchunguzi wa matukio ya uvunjifu wa amani yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, akisema imefanya kazi ya kizalendo na ya kisayansi.
Aidha mwenyekiti huyo aliwataka Watanzania kuwa wavumilivu wakati serikali ikitekeleza mapendekezo ya Ripoti ya Tume ya Uchunguzi wa matukio ya uvunjifu wa amani ya Oktoba 2025.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Hamad Rashid amesema ripoti hiyo imemulika kwa uwazi maeneo ambayo taifa lilikosea na kutoa dira ya namna ya kurekebisha makosa hayo ili kusonga mbele.
Mwenyekiti huyo amesisitiza kuwa ripoti hiyo ni daraja muhimu kuelekea maridhiano ya kitaifa. Amesema kwa sasa kila Mtanzania mwenye nia njema anapaswa kuweka kando tofauti za kisiasa na kujikita katika ujenzi wa umoja.
"Rais amesema kuvunjika kwa koleo sio mwisho wa uhunzi. Tunapaswa kukubali matokeo ya ripoti hii na kufanya kazi ya kujenga nchi yetu. Tatizo letu Watanzania tuna haraka sana, tunahitaji kuwa wavumilivu wakati mipango na programu za utekelezaji zikifanyiwa kazi," alisema Hamad Rashid.
Hamad Rashid amebainisha kuwa tume hiyo imetumia weledi mkubwa na mbinu za kisayansi ambazo zimesaidia kupata ukweli wa mambo, ikiwemo madai ya kuwepo kwa makaburi ya pamoja.
"Kuna suala la makaburi ya pamoja ambalo lilikuwa likivuma, lakini uchunguzi wa kisayansi umegundua kuwa madai hayo si ya kweli. Hili ni jambo kubwa ambalo limeondoa taharuki na kuleta ukweli mbele ya jamii," aliongeza.
Akirejea historia ya nchi, Hamad Rashid amekumbusha machafuko ya mwaka 2001 yaliyozalisha wakimbizi zaidi ya 2,000, lakini jitihada za kuketi meza moja zilipelekea kupatikana kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) Zanzibar.
Amesema Katiba na maridhiano ni mambo yanayohitaji busara, huku akibainisha kuwa kuna zaidi ya watu 700 waliopata athari za kisaikolojia ambao hivi sasa wanapatiwa matibabu, jambo ambalo ni hatua muhimu katika kuiponya jamii.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment