" BENKI YA CRDB YATANGAZA ONGEZEKO LA FAIDA NA GAWIO KWA MWANAHISA

BENKI YA CRDB YATANGAZA ONGEZEKO LA FAIDA NA GAWIO KWA MWANAHISA

Benki ya CRDB imetangaza neema kwa wanahisa kwa ongezeko la asilimia 38 kutoka sh.65 ya mwaka jana hadi kufikia sh.90 kwa hisa moja mwaka huu.Akizungumza na waandishi wa habari kuelekea mkutano mkuu wa 31 wa wanahisa Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa benki ya CRDB Prof. Neema Mori amesema wanahisa wana mchango mkubwa na ni nguzo ya msingi katika maendeleo endelevu.Aidha amewakaribisha wanahisa kuhudhuria kwa wingi katika semina na mkutano mkuu wa 31 ili kujifunza, kuweka mikakati ya pamoja, kutambua fulsa zilizopo, kukaribisha wanahisa wapya na kufahamishwa fulsa mpya.Vilevile amesisitiza kuwa vijana ndio nguvu ya uwekezaji katika taifa lolote duniani. Kupitia semina hiyo vijana wameandaliwa fulsa mpya ya uwezeshwaji katika uwekezaji kuhakikisha wanamiliki uchumi mzuri."Mkutano huu ni muhimu sana kwetu, wadau, wananchama na wanahisa kwa ujumla, tutakuwa na mada 12 za msingi ambazo zitatuvusha kufikia mafanikio yetu kwa pamoja, endeleeni kuiamini benki ya CRDB kwa sababu inazingatia misingi na kanuni" amesema Prof.Neema.Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB Dkt. Abdulmajid Nsekela amesema benki hiyo imeendelea kuwa imara na kufanikiwa kuvuna faida ya shilingi bilioni 206 kwa kipindi cha mwaka mmoja.Hata hivyo ameongeza kuwa, ubunifu umeongezeka, na huduma nyingi kwa sasa zinapatikana nje ya benki. Mafanikio ya miaka 30 ijayo yanategemea uwekezaji wa kina kwa vijana wa sasa, tutahakikisha tunakuwa nao karibu ili kuandaa wawekezaji wazuri wa kesho. "Benki yetu imevuka mipaka na imeendelea kufanya vizuri kimataifa, nawashukiru sana wateja wetu kutuamini na kuwekeza kwetu,  Kama kampuni inayomilikiwa kwa mfumo wa hisa, wanahisa wana nafasi ya kupata taarifa, kutoa maoni na  kufahamu mustakabali wa benki yao,  Wito wangu kwenu vijana changamkieni fulsa ambazo benki yenu imewaletea ili kesho muwe wawekezaji wakuu wa CRDB" amesema Dkt. Nsekela.

 SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post