" BONANZA LA MICHEZO WANAFUNZI WA KIKE LAFANA FUNGUNI SEKONDARI

BONANZA LA MICHEZO WANAFUNZI WA KIKE LAFANA FUNGUNI SEKONDARI


NA: MWANDISHI WETU, PANGANIUongozi wa Shule kwa kushirikiana na Idara ya Michezo katika Shule ya Sekondari Funguni ya wilayani Pangani mkoani Tanga, umeratibu Bonanza la Michezo kwa wanafunzi wa kike waishio hosteli ikiwa ni njia ya kuhimiza ushirikiano, furaha, kujenga afya, kuibua na kukuza vipaji miongoni mwa wanafunzi.Bonanza hilo limefanyika Mei 30, 2026, katika uwanja wa shule. Bonanza limejumuisha michezo mbalimbali ikiwemo riadha ya umbali wa mita 100 na 400, kuruka na mpira wa miguu.Katika mbio za mita 100, walioibuka washindi ni Fatuma  Selemani, Mary Yoram, Veronica Michael na Elizabeth Paschal.Aidha, katika mbio za mita 400, washindi ni Zakatu Ramadhani, Rebeca Ngoda na Zainabu Shabani.Aidha, katika mchezo wa kuruka, washindi ni Irene Daniel na Fatuma Selemani.Katika hatua nyingine, Bonanza hilo pia lilijumuisha mechi ya mpira wa miguu ya timu ya wasichana ya Bweni A na Bweni B.Timu ya Bweni A iliibuka kidedea kwa kupata ushindi mnono wa magoli (6-0) dhidi ya Bweni B. Akizungumzia Bonanza hilo, Mkuu wa Shule, Nassoro Gamba alisema michezo ni muhimu kwa wanafunzi na inasaidia kuwajenga kiafya na kiakili."Huu ni mwanzo tu, kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi, tutakuwa na Bonanza la Michezo. Leo nimejiona vipaji vikubwa sana kwa wanafunzi wangu. Funguni Sekondari tunahimiza taaluma na michezo pia," amesema Gamba.Kwa upande wa mwalimu wa michezo wa shule hiyo, Isihaka Shekalaghe, amewahimiza wanafunzi kufanya mazoezi mara kwa mara, na huku akiwaahidi kuwapa kila aina ya ushirikiano wanaoutaka ili kukuza vipaji vyao.Katika Bonanza hilo, washindi walipewa zawadi za soda huku Bonanza lijalo, zawadi ya mbuzi ikitarajiwa kutolewa kwa washindi.Kwa upande wa wanafunzi, wamepongeza Bonanza hilo, huku wakisisitiza liwe endelevu.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

 

Post a Comment

Previous Post Next Post