Na Mapuli Kitina Misalaba
Timu ya SONGAMBELE MHANGU kutoka kata ya Salawe
imeendelea kuonesha ubora wake katika mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 baada
ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya SHILIMA FC kutoka Mkoa wa Mwanza
katika mchezo wa marudiano uliochezwa kwenye uwanja wa Mwabenda kata ya Solwa,
Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Ushindi huo umeihakikishia SONGAMBELE MHANGU tiketi ya
kusonga mbele katika hatua inayofuata ya mashindano hayo huku safari ya SHILIMA
FC ikifikia tamati rasmi.
Ikumbukwe kuwa katika mchezo wa kwanza uliochezwa kati
ya timu hizo, SONGAMBELE MHANGU iliibuka na ushindi wa bao 1-0, hivyo kufikisha
jumla ya mabao 5-0 katika michezo yote miwili ya hatua ya mtoano.
Kutokana na ushindi huo, SONGAMBELE MHANGU sasa
itakutana na DUARA FC katika hatua inayofuata ya mashindano hayo baada ya DUARA
FC kufuzu jana dhidi ya MWANDUTU FC.
Baada ya mchezo huo, Katibu wa Kamati ya Mashindano
Sambayi Jilya ametangaza ratiba ya mchezo wa kesho ambapo NZOZA FC itamenyana
na NYUNDO FC katika pambano linalotarajiwa kuvuta hisia za mashabiki wengi wa
soka ndani na nje ya kata ya Solwa.
Sambayi amewahimiza wananchi, wadau wa michezo pamoja
na mashabiki wa timu hizo kujitokeza kwa wingi katika uwanja wa Mwabenda ili
kuendelea kushuhudia michezo yenye ushindani mkubwa na vipaji vinavyochipukia
kupitia mashindano hayo.
Mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 yameandaliwa na
Bwana Paul Daud Augustino maarufu MC NIACHEKONA kupitia ufadhili wa shirika la Lushu
Foundation yakiwa na lengo la kuibua vipaji vya vijana, kukuza michezo,
kuimarisha amani na kuleta mshikamano katika jamii.
Kwa huduma za ushereheshaji wa shughuli mbalimbali,
matangazo na matukio ya kijamii, MC NIACHEKONA anapatikana kupitia namba 0757
267 738.
Kikosi cha Songambele Mhangu FC.
Wachezaji wa SONGAMBELE MHANGU na SHILIMA FC wakioneshana uwezo mkubwa katika mchezo wa marudiano wa NIACHEKONA CUP 2026 uliochezwa uwanja wa Mwabenda kata ya Solwa leo Jumamosi Mei 30, 2026.
SHILIMA FC wakijaribu kutafuta bao la kufufua matumaini yao katika mchezo wa leo wa NIACHEKONA CUP 2026.
Mashabiki wa soka wakifuatilia kwa hamasa kubwa mchezo kati ya SONGAMBELE MHANGU na SHILIMA FC katika uwanja wa Mwabenda.
Mashabiki wa soka wakifuatilia kwa hamasa kubwa mchezo kati ya SONGAMBELE MHANGU na SHILIMA FC katika uwanja wa Mwabenda.
Mashabiki wa soka wakifuatilia kwa hamasa kubwa mchezo kati ya SONGAMBELE MHANGU na SHILIMA FC katika uwanja wa Mwabenda.
Sehemu ya wananchi waliojitokeza kwa wingi kushuhudia mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 yanayoendelea kata ya Solwa.
Mashabiki wa soka wakionesha mapenzi yao kwa mchezo kwa kujitokeza kwa wingi kushuhudia vipaji vya vijana.
Mashabiki wa soka wakionesha mapenzi yao kwa mchezo kwa kujitokeza kwa wingi kushuhudia vipaji vya vijana.
Burudani ya soka ikiendelea katika uwanja wa MwabendaSHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254















Post a Comment