" DKT. DOROTHY GWAJIMA AMPONGEZA ASKARI NA MSANII NYUMBU MJANJA KWA KUTOA ELIMU KUPITIA SANAA

DKT. DOROTHY GWAJIMA AMPONGEZA ASKARI NA MSANII NYUMBU MJANJA KWA KUTOA ELIMU KUPITIA SANAA

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima, amempongeza askari wa Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga na msanii wa Hip Hop, Nyumbu Mjanja (CPL Gabriel Kayaga), kwa kutumia sanaa yake kufikisha ujumbe wa elimu kwa wanafunzi.

Dkt. Gwajima alitoa pongezi hizo kufuatia ubunifu wa msanii huyo ambaye amekuwa akitumia muziki na maonesho yake kuhamasisha wanafunzi kuhusu umuhimu wa elimu, maadili na kujitambua.

Alisema matumizi ya sanaa katika kutoa elimu ni njia yenye ufanisi mkubwa, hasa kwa vijana, kwani huwavutia na kuwafanya kupokea ujumbe kwa urahisi zaidi.

Nyumbu Mjanja ambaye pia ni askari wa Polisi mkoa wa Shinyanga, wakati akizungumza na Misalaba Media, amesema ataendelea kutumia sanaa yake kama chombo cha kuleta mabadiliko chanya katika jamii, hususan kwa vijana na wanafunzi.

Hatua hiyo imepongezwa na wadau mbalimbali wakieleza kuwa ushirikiano kati ya viongozi na wasanii unaweza kusaidia kuimarisha utoaji wa elimu kwa njia bunifu na yenye mvuto kwa kizazi cha sasa.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

 

Post a Comment

Previous Post Next Post