" INEC YATOA VIBALI KWA TAASISI ZA KIRAIA KUTOA ELIMU YA MPIGA KURA NA UANGALIZI UCHAGUZI MDOGO ISMANI

INEC YATOA VIBALI KWA TAASISI ZA KIRAIA KUTOA ELIMU YA MPIGA KURA NA UANGALIZI UCHAGUZI MDOGO ISMANI

 

Morogoro — Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imetoa kibali kwa taasisi na asasi za kiraia tatu (03) kushiriki katika utoaji wa elimu ya mpiga kura wakati wa Uchaguzi Mdogo wa Ubunge katika Jimbo la Ismani, Halmashauri ya Wilaya ya Iringa pamoja na kata 12 za Tanzania Bara.

Uamuzi huo umetolewa katika kikao cha Tume kilichofanyika Mei 1, 2026, kwa mujibu wa kifungu cha 10(1)(h) cha Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 292, kikisomwa pamoja na kanuni ya 22(4) ya Kanuni za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi za mwaka 2024.

Katika hatua nyingine, Tume hiyo imetoa pia kibali kwa taasisi na asasi za kiraia za ndani ya nchi mbili (02) kuwa waangalizi wa uchaguzi huo mdogo, kwa mujibu wa kifungu cha 85(4) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Sura ya 343 pamoja na kanuni ya 13(4) ya Kanuni za Uchaguzi za mwaka 2025.

Tume imezipongeza taasisi zote zilizopata vibali hivyo, ikieleza kuwa ushiriki wao ni muhimu katika kuimarisha uelewa wa wananchi kuhusu mchakato wa uchaguzi pamoja na kuongeza uwazi na uaminifu katika uchaguzi huo mdogo wa Jimbo la Ismani na kata husika.

Post a Comment

Previous Post Next Post