
Na Mapuli Kitina Misalaba
Mdau wa michezo na mwandaaji wa mashindano ya
NIACHEKONA CUP 2026, Bwana Paul Daud Augustino amesema mashindano hayo yamelenga
kuleta hamasa kubwa kwa vijana huku wadhamini mbalimbali wakitumia nafasi hiyo
kutoa ujumbe wa maendeleo na kuwahimiza wananchi kujikita katika shughuli za
uzalishaji mali.
Akizungumza katika muendelezo wa mashindano hayo
yanayoendelea katika uwanja wa Mwabenda kata ya Solwa, MC NIACHEKONA amesema
wadhamini wake wameendelea kusimama bega kwa bega kuhakikisha ligi hiyo
inafanikiwa huku ikibeba ujumbe wa kuwakutanisha vijana kupitia michezo.
Amesema mfadhili wake Mabula Lushu wa Mahembe
ameendelea kutoa hamasa kwa vijana kwa kuwakumbusha umuhimu wa kufanya kazi kwa
bidii kabla ya kujihusisha na burudani au vijiwe vya mazungumzo.
“Mabula Lushu anawakumbusha vijana kwamba
maisha yanahitaji kazi kwanza. Kama wewe ni mkulima, mfugaji au mfanyabiashara
hakikisha unatimiza majukumu yako kwa bidii ili uwe sehemu ya maendeleo ya
jamii na taifa kwa ujumla,” amesema MC NIACHEKONA.
Ameongeza kuwa Mabula Lushu ambaye ni mkulima na
mfugaji ameonesha dhamira ya kuwasaidia vijana kwa kutumia michezo kama sehemu
ya kuwajenga na kuwaweka karibu na shughuli za maendeleo.
Aidha amesema mdhamini mwingine ambaye ni Jambo FM
kupitia kipindi chake cha michezo ameendelea kuwafikishia wananchi taarifa
mbalimbali kuhusu mwenendo wa mashindano hayo huku akiwahamasisha wananchi
kuendelea kufuatilia vipindi vya michezo vinavyorushwa kila siku kuanzia saa
moja na nusu.
“Jambo FM wanawakumbusha wananchi
kuhakikisha wanaendelea kusikiliza vipindi vya michezo ili kupata taarifa
mbalimbali za NIACHEKONA CUP pamoja na maendeleo ya ligi hii,”
amesema.
Pia amesema Misalaba
Media inaendelea kurusha matukio ya mashindano hayo kupitia majukwaa ya
kidijitali ikiwemo YouTube na Instagram ambapo wananchi wamekuwa wakipata
habari, matokeo na matukio mbalimbali ya michezo hiyo.
MC NIACHEKONA ameendelea kuwakaribisha wananchi wa
Solwa na maeneo jirani kujitokeza kwa wingi kila siku kuanzia saa kumi jioni
katika uwanja wa Mwabenda kushuhudia burudani ya soka pamoja na vipaji vya
vijana vinavyoendelea kuibuliwa kupitia mashindano hayo.
Mbali na kuwa mwandaaji wa mashindano hayo, Paul Daud
Augustino ni mdau mkubwa wa michezo katika Wilaya ya Shinyanga ambaye amekuwa
mstari wa mbele kusaidia timu mbalimbali pamoja na kuandaa mashindano ya
vijana, huku NIACHEKONA CUP 2026 ikiwa ni ligi yake ya tatu kuandaa mwaka huu.
Kwa huduma za ushereheshaji wa shughuli mbalimbali, zikiwemo za kijamii na matukio tofauti wasiliana na MC NIACHEKONA kupitia namba 0757 267 738.

Wachezaji wa NYUNDO FC na NZOZA wakioneshana uwezo katika mchezo wa NIACHEKONA CUP 2026 uliomalizika kwa sare ya bao 1-1 kwenye uwanja wa Mwabenda kata ya Solwa.
Mchezo ukiendelea katika uwanja wa Mwabenda ambapo NYUNDO FC na NZOZA ziligawana pointi baada ya kutoka sare ya bao 1-1.
Baadhi ya viongozi pamoja na wadau wa michezo wakifuatilia kwa karibu mchezo wa NYUNDO FC dhidi ya NZOZA katika mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 uwanja wa Mwabenda kata ya Solwa.
Sehemu ya wananchi wakifuatilia kwa hamasa mchezo wa NYUNDO FC dhidi ya NZOZA uliovutia mashabiki wengi.
Sehemu ya wananchi wakifuatilia kwa hamasa mchezo wa NYUNDO FC dhidi ya NZOZA uliovutia mashabiki wengi.
Wachezaji wakipambana kuwania mpira katika mchezo wa ushindani mkubwa wa NIACHEKONA CUP 2026 uliochezwa Solwa.
Wachezaji wakipambana kuwania mpira katika mchezo wa ushindani mkubwa wa NIACHEKONA CUP 2026 uliochezwa Solwa.
Sehemu ya wananchi wakifuatilia kwa hamasa mchezo wa NYUNDO FC dhidi ya NZOZA uliovutia mashabiki wengi.
Sehemu ya wananchi wakifuatilia kwa hamasa mchezo wa NYUNDO FC dhidi ya NZOZA uliovutia mashabiki wengi.Mchezo ukiendelea katika uwanja wa Mwabenda ambapo NYUNDO FC na NZOZA ziligawana pointi baada ya kutoka sare ya bao 1-1.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254







































Post a Comment