" NIACHEKONA CUP YATAJWA KUIMARISHA AFYA YA AKILI NA MWILI, WATAKA MC NIACHEKONA APEWA SAPOTI ZAIDI KUTIMIZA NDOTO ZA VIJANA

NIACHEKONA CUP YATAJWA KUIMARISHA AFYA YA AKILI NA MWILI, WATAKA MC NIACHEKONA APEWA SAPOTI ZAIDI KUTIMIZA NDOTO ZA VIJANA

Na Mapuli Kitina Misalaba

Baadhi ya wadau wa michezo katika kata ya Solwa, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wamepongeza mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 wakisema yamekuwa na mchango mkubwa katika kuimarisha afya ya akili na mwili kwa vijana pamoja na wananchi wanaofuatilia michezo hiyo.

Wakizungumza na Misalaba Media, wadau hao wamesema michezo ni nyenzo muhimu ya kujenga afya bora, kuimarisha mshikamano wa jamii na kuwasaidia vijana kutumia muda wao katika shughuli zenye manufaa.

Wamempongeza mwandaaji wa mashindano hayo, Bwana Paul Daud Augustino maarufu MC NIACHEKONA, kwa juhudi zake za kuendeleza michezo na kuibua vipaji vya vijana kupitia mashindano hayo yanayoendelea katika uwanja wa Mwabenda.

Aidha, wamemshauri kuangalia uwezekano wa kuanzisha timu au programu ya mbio za jogging ili kuwapa wananchi na vijana fursa zaidi za kushiriki shughuli za mazoezi na kuimarisha afya zao.

Wadau hao pia wamewaomba wadau wengine wa maendeleo, wafadhili na wadau wa michezo kuendelea kumuunga mkono MC NIACHEKONA ili vijana wengi zaidi waweze kunufaika na michezo kama sehemu ya ajira, ukuzaji wa vipaji na maendeleo ya kijamii.

Sambamba na hilo, wamewahimiza wafanyabiashara na wajasiriamali kutumia fursa ya mashindano hayo kwa kufika katika uwanja wa Mwabenda wakati wa mechi zinazoendelea kila siku jioni ili kuuza bidhaa na huduma mbalimbali, hatua ambayo inaweza kuongeza kipato chao na kuchangia ukuaji wa uchumi wa eneo hilo.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post