" PUUZENI UONGO WA MITANDAONI KUHUSU BUNGE LA ULAYA NA RAIS SAMIA

PUUZENI UONGO WA MITANDAONI KUHUSU BUNGE LA ULAYA NA RAIS SAMIA

 

erikali kupitia Idara ya Habari-MAELEZO imetoa kanusho dhidi ya taarifa inayosambazwa mitandaoni ikidai kuwa Bunge la Ulaya limetoa maazimio ya kuondolewa kwa nguvu kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.

 Idara hiyo imebainisha wazi kuwa taarifa hizo ni uongo na upotoshaji unaopikwa na baadhi ya wanaharakati wa mitandaoni kwa lengo la kuzua taharuki isiyo na msingi miongoni mwa jamii. 

Taarifa hiyo ilisema kwamba Video inayotumika kusambaza uongo huo ni ya tarehe 26 Novemba, 2025, na haihusiani kabisa na madai yanayotolewa, kwani Bunge la Ulaya haliendeshi mjadala wowote wa aina hiyo wala hakuna maazimio kama hayo yaliyofikiwa dhidi ya Tanzania.

Aidha taarifa hiyo imewataka wananchi kupuuza uongo huo wa mitandaoni ambao una dhima ya wazi ya kukwamisha juhudi kubwa zinazofanywa na Watanzania katika kuleta mshikamano, maridhiano, na kuondoa chuki miongoni mwetu. 

"Serikali inaendelea kuwasihi Watanzania wote kuepukana na usambazaji wa taarifa hizi za upotoshaji ambazo zinachochea mifarakano na kudhoofisha umoja wa kitaifa. 

Ni muhimu kwa kila mwananchi kuwa mzalendo na kulinda amani iliyopo kwa kutozingatia uvumi unaolenga kurudisha nyuma hatua za maridhiano zilizofikiwa kwa maslahi ya taifa zima." ilisema sehemu ya taarifa hiyo. 

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post