" SAFARI YA GRIDI YA TAIFA YA MAJI IMEANZA, WANANCHI TUTUNZE VYANZO VYA MAJI KWA MAENDELEO

SAFARI YA GRIDI YA TAIFA YA MAJI IMEANZA, WANANCHI TUTUNZE VYANZO VYA MAJI KWA MAENDELEO


NA: DK. REUBENI LUMBAGALANi dhamira ya kweli ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kumtua mama ndoo kichwani yaani kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji katika makazi yao na kuepukana na kadhia ya kuchota maji umbali mrefu.Kwa lugha rahisi ni kwamba, Dk. Samia anataka wananchi wote wapate maji kwa asilimia mia moja. Kwa kuzingatia umuhimu wa maji, katika maisha na maendeleo ya binadamu, ni muhimu kuhakikisha huduma hiyo inawafikia wananchi wote.Tanzania imebarikiwa kuwa na vyanzo vingi vya maji ambavyo mikakati madhubuti ikiwekwa, vinaweza kumaliza changamoto ya upatikanaji wa maji kwa wananchi. Rais Dk. Samia akiwa mdau muhimu wa sekta ya maji, huku akichukizwa na namna wananchi wakiwemo wanawake na watoto wakitembea umbali mrefu kutafuta maji, ameipa Wizara ya Maji jukumu la kuhakikisha inatekeleza mradi wa Gridi ya Taifa ya Maji.Rais Dk. Samia ametolea mfano Wizara ya Nishati ilivyo na Gridi ya Taifa ya Umeme, ndivyo Wizara ya Maji inapaswa kuwa na Gridi ya Taifa ya Maji. GRIDI YA TAIFA YA MAJI NI NINI?Ni mfumo wa kitaifa unaounganisha miundombinu ya maji kutoka vyanzo vikubwa vya maji vya uhakika kama maziwa na mito ili kusambaza maji safi na salama kwa matumizi mbalimbali kwa maendeleo.Kupitia mradi huo, maji yatatolewa Ziwa Viktoria kuelekea mikoa ya Shinyanga, Singida, Dodoma, Kilimanjaro, Manyara na Arusha. Kutoka Ziwa Nyasa, maji yatapelekwa mikoa ya Ruvuma, Lindi, Mtwara, Njombe, Iringa, na Mbeya.Vilevile, maji yatatoka Ziwa Tanganyika kuelekea mikoa ya Kigoma, Tabora, Katavi, Rukwa na Songwe.Kama hiyo haitoshi, Mto Rufiji nao utasaidia kupeleka maji mikoa ya Pwani, Dar es Salaam, Tanga na Morogoro.Hii yote ni kuhakikisha maji yanatolewa kutoka vyanzo vikubwa vya maji kama mito na maziwa na kuwafikia wananchi wote vikiwemo vijiji 1,575 vilivyosalia ifikapo mwaka 2030.VIONGOZI NA WATENDAJI WA MAJI WAFANYA ZIARA CHINA KUJIFUNZA GRIDI YA TAIFA YA MAJI Mwezi Machi, 2026, timu kutoka Wizara ya Maji wakiongozwa na Waziri wake, Jumaa Aweso, Katibu Mkuu Mhandisi Mwajuma Waziri na watendaji wengine, walifanya ziara ya mafunzo nchini China katika Jimbo la Shan Dong kujifunza namna ambavyo vyanzo vikubwa vya maji na maziwa vimeunganishwa katika Gridi ya Taifa ya Maji kutoka Kaskazini kwenda Kusini mwa China.Mafunzo hayo ni muhimu wakati huu ambao  wataalamu wanahitaji uelewa kufanikisha usambazaji wa maji kutoka Ziwa Viktoria, Nyasa na Tanganyika. Pia, kutoka mito mikubwa ya Kagera, Rufiji, Ruvu, Wami, Ruvuma, Pangani na Kiwira ili yawafikie wananchi walipo kwa maendeleo. MFUMO WA UTABIRI WA KIASI CHA MAJI KWENYE MITO WAZINDULIWAMachi 22, 2026, ikiwa ni Siku ya Kilele cha Wiki ya Maji nchini na Siku ya Maji Duniani, Makamu wa Rais, Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, alizindua Mfumo wa Utabiri wa Kiasi cha Maji kwenye Mito, Morogoro Mjini.Aidha, mfumo huu utawezesha kupata taarifa sahihi za kiwango cha maji tulichonacho nchini ili kufanikisha mahitaji ya maji katika shughuli mbalimbali za maendeleo hasa kuelekea Dira ya Maendeleo ya mwaka 2050, ambapo Tanzania inakadiriwa itakuwa na watu milioni 118.WABUNGE WAJENGEWA UWEZO MRADI GRIDI YA TAIFA YA MAJIHivi karibuni, wabunge katika Ukumbi wa Pius Msekwa Jijini Dodoma, walipewa semina kuhusiana na utekelezaji wa mradi wa Gridi ya Taifa ya Maji ikizingatia kuwa mradi huo unagusa majimbo na wananchi wao.Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri aliwaeleza wabunge mradi huo mkubwa namna utakavyowanufaisha wananchi na Taifa kwa ujumla. Aidha, wabunge walipewa taarifa kuhusiana na kukamilika kwa vipande vya mtandao wa taifa wa maji ambapo tayari maji yameanza kutolewa Ziwa Viktoria kuelekea Shinyanga, Tabora na maeneo ya Shelui mkoani Singida.WANANCHI NA WAJIBU WA KUTUNZA VYANZO VYA MAJIWananchi tunao wajibu wa kulinda vyanzo vya maji ili kuhakikisha tunapata maji safi, salama na yenye kutosheleza kwa mahitaji ya maendeleo. Kimsingi, vyanzo vya maji vinapaswa kulindwa. Iko hivi: Walinzi wa kwanza wa vyanzo hivi ni sisi wananchi. Wananchi ndiyo wanufaika wa kwanza wa maji, kwahiyo, namna zozote za uhujumu na uharibifu wa vyanzo vya maji, ni kujidhulumu sisi wenyewe na kuchelewesha utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo ambazo zinarudisha nyuma kasi ya maendeleo.Sambamba na hilo, wananchi tunao wajibu wa kutoa taarifa kwenye mamlaka husika kuhusu upotevu wa maji pale tunapoona maji yanamwagika na wizi wa maji unaofanywa na baadhi ya watu wasio waaminifu.Kwa pamoja, tunaweza kufanikisha mipango mingi ya maendeleo katika sekta za kilimo, uvuvi, viwanda, miundombinu kama tutatunza vyanzo vya maji kwa maendeleo hasa kuelekea Dira ya Maendeleo ya mwaka 2050 ambapo sekta ya maji ina sehemu kubwa kufanikisha mipango hiyo mizuri ya maendeleo.

 SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post