" SERIKALI MBIONI KUONGEZA UWEKEZAJI WAKUNGA

SERIKALI MBIONI KUONGEZA UWEKEZAJI WAKUNGA

Na, Belnardo Costantine.Serikali kupitia Wizara ya Afya imejipanga kuendelea kuongeza uwekezaji katika mafunzo, ajira, motisha na mazingira ya kazi kwa wakunga kwa lengo la kuzidi kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa Watanzania.Taarifa hiyo imetolewa  na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe,Mei 2, 2026  katika Maadhimisho ya siku ya Mkunga Duniani yaliyofanyika kitaifa Mkoani Kilimanjaro. "Nitoe wito kwa wakunga wote nchini kuendelea kutoa huduma za afya kwa weledi, juhudi na kuzingatia maadili ya taaluma zao ili kuhakikisha usalama wa mama na mtoto unaimarika," amesema Dkt. ShekalagheAidha amesema, hatua kali zitachukuliwa kwa watakaokiuka maadili ya taaluma huku akisisitiza kuwa, Serikali haitasita kuwawajibisha watoa huduma watakaotoa huduma kinyume na viwango vinavyotakiwa, ili kulinda hadhi ya taaluma na usalama wa wagonjwa.Sambamba na Hilo Dkt. Shekalaghe ameihimiza jamii kutumia huduma zinazotolewa kwenye vituo vya afya ili kupata huduma sahihi kutoka kwa wakunga wataalamu badala ya kujifungulia nyumbani bila uangalizi wa kitaalamu huku akihimiza ushirikiano kati ya jamii na watoa huduma ni muhimu hasa wakati wa dharura, Katika hatua nyingine, Dkt. Shekalaghe ameitaka jamii kuwaunga mkono wakunga kwa kuwaheshimu, kushirikiana nao na kuhakikisha wanapata huduma za afya mapema na kwa wakati.“Serikali inatambua mchango wenu wakunga kwa kazi kubwa mnayoifanya, Tuzo aliyotunukiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya 'Goalkeeper' kama kinara wa kupunguza vifo vya mama na mtoto, lakini pia kuchaguliwa kwake kuwa Kinara wa masuala ya mama na mtoto Afrika, ni dhahiri ya juhudi na utendaji kazi wenu bora, hivyo nawapongeza sana” amesema Dkt. ShekalagheVilevile, Dkt. Shekalaghe amesisitiza kuwa, wadau wa sekta ya afya kushiriki kikamilifu katika kuboresha huduma za afya ya uzazi na kuweka mazingira bora yatakayowawezesha wakunga kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi. Hata hivyo Akizungumzia Wakunga Marathon iliyoenda sambamba na maazimisho ya siku ya mkunga,Dkt. Shekalaghe amewapongeza washiriki kwa kutumia michezo kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa afya ya mama na mtoto, akisisitiza kuwa kuwawezesha wakunga ni hatua muhimu ya kuokoa maisha.

Post a Comment

Previous Post Next Post