" WANANCHI WAFUNGUKA UMUHIMU WA MICHEZO, WAIPONGEZA NIACHEKONA CUP

WANANCHI WAFUNGUKA UMUHIMU WA MICHEZO, WAIPONGEZA NIACHEKONA CUP

Na Mapuli Kitina Misalaba

Baadhi ya wananchi wa kata ya Solwa na maeneo jirani wamezungumzia umuhimu wa michezo katika jamii wakisema imeendelea kuwa nyenzo muhimu ya kuimarisha afya, amani, mshikamano pamoja na maendeleo ya vijana.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika uwanja wa Mwabenda, wananchi hao wamesema michezo imekuwa ikiwakutanisha watu kutoka maeneo mbalimbali na kuwapa nafasi ya kubadilishana uzoefu, kujenga urafiki na kuimarisha mahusiano miongoni mwao.

Wameeleza kuwa vijana wengi wanaposhiriki michezo au kufuatilia mashindano mbalimbali hupata fursa ya kutumia muda wao katika shughuli zenye manufaa badala ya kujihusisha na vitendo vinavyoweza kuhatarisha mustakabali wao na maendeleo ya jamii.

Aidha wamesema michezo ni sehemu ya ajira na uchumi kwani huwasaidia wafanyabiashara, waendesha bodaboda, mama lishe na makundi mengine ya kijamii kupata kipato kupitia mikusanyiko ya watu wanaofika kushiriki au kushuhudia michezo.

Wananchi hao pia wamepongeza mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 yanayoendelea katika uwanja wa Mwabenda kwa kuendelea kutoa nafasi kwa vijana kuonesha vipaji vyao huku yakihamasisha amani, umoja na mshikamano katika jamii.

Wamempongeza mwandaaji wa mashindano hayo, Bwana Paul Daud Augustino maarufu MC NIACHEKONA kwa juhudi zake za kuendeleza michezo katika eneo hilo na kuwapa vijana jukwaa la kuonesha uwezo wao.

Wamewataka wadau mbalimbali wa michezo kuendelea kuunga mkono mashindano hayo ili yaweze kukua zaidi na kuwafikia vijana wengi wanaohitaji fursa za kuonesha vipaji vyao.

Hadi sasa baadhi ya timu zilizofanikiwa kutinga hatua inayofuata ya mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 ni pamoja na HOME BOYS, WAFUKUNYUNGU FC, DUARA FC na SONGAMBELE MHANGU huku timu nyingine zikiendelea kupambana kutafuta nafasi ya kuungana nazo katika hatua inayofuata ya mashindano hayo.

Kwa huduma za ushereheshaji wa shughuli mbalimbali, matangazo na matukio ya kijamii, MC NIACHEKONA anapatikana kupitia namba 0757 267 738.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

 

Post a Comment

Previous Post Next Post