" WAUGUZI WAPONGEZWA UTENDAJI IMARA NA NGUZO MUHIMU SEKTA YA AFYA NCHINI

WAUGUZI WAPONGEZWA UTENDAJI IMARA NA NGUZO MUHIMU SEKTA YA AFYA NCHINI


Na,Egidia Vedasto,Misalaba Media, Arusha.Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeendelea kuboresha sekta ya afya nchini kwa kuongeza vifaa, vifaa tiba pamoja na kuboresha maslahi ya watumishi wa afya ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora wakati wote.Serikali imesisitiza kuwa wauguzi ni sehemu muhimu katika utoaji wa huduma za afya nchini.Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Wauguzi Duniani Jijini Arusha, Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Regina Ndege Qwaray  ameeleza kuwa serikali imepokea mapendekezo ya chama cha Wauguzi na itaendelea kuboresha muundo wa kazi.Aidha, amewataka wauguzi kuendelea kutoa huduma zenye staha, upendo na huruma kwa wagonjwa, kuepuka lugha zisizo na faraja akisisitiza kuwa maisha ya wagonjwa yako mikononi mwao."kazi ya uuguzi ni wito wenye thamani kubwa mbele ya jamii na Mungu, hivyo wauguzi mnapaswa kuwa karibu na wagonjwa ili kusaidia kuzuia vifo visivyo vya lazima. Serikali ina imani kubwa kwa kada yenu kutokana na mchango wenu mkubwa katika kuokoa maisha ya wananchi" amesema Qwaray.Kwa upande wake, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Jafar Seif amesema serikali itaendelea kuimarisha sekta ya afya katika ngazi ya msingi ikiwemo ujenzi wa miundombinu, upatikanaji wa vifaa tiba na huduma za uchunguzi."Sisi sote ni mashahidi kwamba maboresho katika hospitali hata vituo vya afya ni makubwa, vifaa vya uchunguzi zimeongezwa, miundo mbinu kwa ujumla ni safi, hatua hii imesaidia sana kuokoa maisha ya mama na mtoto.Katibu Tawala wa Wilaya ya Arusha, Dkt.Jacob Rombo, aliyemwakilisha Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, amesema serikali itaendelea kushughulikia changamoto zinazowakabili wauguzi, ikiwemo kuboresha mazingira na maslahi yao ya kazi. Ameeleza kuwa huduma za wauguzi zimekuwa msingi mkubwa wa kuokoa afya za wananchi wengi.Naye Rais wa Chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA), Dkt.Ezekiel Mbao ameiomba serikali kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wauguzi kwa muda mrefu. Wakati huo huo, Mwenyekiti wa TANNA Mkoa wa Arusha, Sista Janeth Ngopa, amewataka wauguzi kuendelea kufanya kazi kwa moyo wa upendo, mshikamano na huruma kwa wagonjwa ili kuenzi misingi ya taaluma ya uuguzi duniani.

 SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment

Previous Post Next Post