Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kasulu Mwl. Vumilia Julius Simbeye amefunga mafunzo kwa vikundi 17 vilivyokidhi vigezo vya kunufaika na mikopo ya asilimia 10 kwa robo ya tatu ya mwaka ambapo zaidi ya shilingi milioni 214 zimetengwa kwa ajili ya kuwezesha vikundi hivyo.Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi mkubwa wa mikutano wa Halmashauri hiyo yakilenga kuwajengea uwezo washiriki kuhusu matumizi sahihi ya mikopo ili kuhakikisha wanafikia malengo waliyojiwekea.Akifunga mafunzo hayo, Mwl. Simbeye amewataka washiriki kutumia vyema elimu waliyoipata ili mikopo hiyo iwe chachu ya maendeleo ya vikundi vyao, akisisitiza umuhimu wa upendo, umoja na uaminifu katika urejeshaji wa mikopo hiyo itakayoendelea kuwanufaisha zaidi wananchi.Kwa upande wao, washiriki wa mafunzo hayo wameishukuru Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, Kitengo cha Maendeleo ya Jamii pamoja na Ofisi ya Mkurugenzi kwa kuwezesha mafunzo hayo wakieleza kuwa elimu waliyoipata itawasaidia katika usimamizi wa fedha, utekelezaji wa majukumu yao ndani ya vikundi na kuchochea maendeleo ya Halmashauri kwa ujumla.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254




Post a Comment