Na Edington Mukiza Ezron, Misalaba Media
Baadhi ya wananchi katika Manispaa ya Shinyanga
wamewataka wazazi na walezi kuzingatia malezi bora kwa watoto wao kwa kuwajenga
katika misingi ya maadili ya Kitanzania ili kulinda heshima ya jamii na taifa
kwa ujumla.
Wakizungumza na Misalaba Media leo Mei 5, 2026,
wananchi hao wamesema baadhi ya wazazi wamekuwa wakilegeza usimamizi wa watoto
wao, hali inayochangia kuporomoka kwa maadili miongoni mwa vijana.
Mzee Aley Juma amesema mmomonyoko wa maadili kwa
vijana unachangiwa na baadhi ya wazazi kufanya vitendo visivyofaa mbele ya
watoto wao, jambo linalowafanya watoto kuiga tabia hizo wanazoziona katika
mazingira yao ya nyumbani.
Aidha, wananchi hao wameeleza kuwa ukosefu wa mbinu
madhubuti za kukemea vitendo visivyofaa katika jamii umechangia vijana wengi
kuendelea kufanya mambo yanayokiuka maadili ya Kitanzania.
Pia wamebainisha kuwa baadhi ya filamu, picha na
maudhui kutoka tamaduni za kigeni, ikiwemo mavazi yasiyoendana na maadili ya
jamii, vimekuwa na athari kwa watoto na vijana, hasa kutokana na matumizi ya
simu na mitandao ya kijamii katika umri mdogo.
Wameongeza kuwa tamaa ya mali na maisha ya kifahari
imewafanya baadhi ya watoto na vijana kujiingiza katika vitendo visivyofaa
kimaadili ikiwemo ukahaba, hali inayohitaji juhudi za pamoja kutoka kwa wazazi,
jamii na serikali.
Hata hivyo, wananchi hao wameiomba serikali kuweka
mikakati madhubuti ya kulinda maadili ya taifa pamoja na kuchukua hatua kali
dhidi ya watu wanaojihusisha na vitendo vinavyokiuka maadili ya jamii.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment