Madiwani wa kata za Halmashauri ya Mji Kasulu wamewasilisha taarifa za utekelezaji wa majukumu yao katika kata zao kwa kipindi cha robo ya tatu ya mwaka kuanzia Januari hadi Machi 2026.Katika uwasilishaji huo, Madiwani wamejikita zaidi kuangazia hali ya usalama, maendeleo ya miradi iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa, ukusanyaji wa mapato na kubainisha changamoto mbalimbali wanazokutana nazo katika maeneo yao.Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya, Katibu Tawala wa Wilaya ya Kasulu Theresia Mtewele amewataka madiwani kuendelea kusimamia hali ya ulinzi na usalama kwa kushirikiana na jeshi la Polisi.Katika hatua nyingine, amewataka Madiwani kufanya kazi kwa kushirikiana na wataalam ili kubaini na kutatua changamoto zinazowakabili wananchi."Madiwani shirikianeni na wataalamu kuwaelimisha wananchi, toeni Elimu kwa changamoto zinazowakabili"Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri Ayubu Ngalaba Kilugu amewataka madiwani kusimamia vyema maeneo yote yaliyo na miradi."Maeneo yote ya miradi niombe sana mkayadhibiti maeneo hayo"Aidha, Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Mwl. Vumilia Julius Simbeye ameahidi kushirikiana kwa karibu zaidi na madiwani ili kuchochea maendeleo."Nipo tayari kushirikiana na madiwani wote kwa muda na wakati wowote ili tuchochee maendeleo ya Kasulu yetu"Suala la ulinzi na usalama linatajwa kuwa chachu muhimu ya kuimarisha maendeleo na ustawi wa wananchi wa Kasulu Mji.



SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

















Post a Comment